Sifa 10 Za Kuangalia Unapomwajiri Mtu Wa Mauzo.

Rafiki yangu mpendwa kuajiri mtu wa mauzo ni hatua muhimu kwa mafanikio ya biashara yako.

Hapa kuna sifa za msingi unazopaswa kuzingatia;

  1. Uwezo wa kuwasiliana. Awe na ustadi mzuri wa kuzungumza na kuandika. Aweze kueleza faida za bidhaa au huduma kwa ufasaha.
  2. Ushawishi na ujuzi wa kujadiliana. Awe na uwezo wa kumshawishi mteja kufanya manunuzi. Aweze kushughulikia upinzani wa mteja kwa busara.
  3. Ujuzi wa mahusiano ya watu. Awe na uwezo wa kujenga na kudumisha mahusiano mazuri na wateja. Awe na tabia ya kirafiki na uvumilivu.
  4. Uelewa wa bidhaa au huduma. Awe na uwezo wa kujifunza haraka kuhusu bidhaa au huduma unazouza. Aweze kueleza thamani ya bidhaa kwa mteja kwa ufanisi.
  5. Uzoefu wa mauzo ( si lazima lakini ni faida). Ikiwezekana awe na uwezo wa kufanya mauzo katika sekta husika. Awe na rekodi nzuri ya kufanikisha mauzo katika kazi za awali.
  6. Motisha ya ndani na bidii. Awe na malengo binafsi na awe tayari kufanya kazi kwa bidii kuyafanikisha. Awe mtu mwenye juhudi na msukumo wa ndani wa kufanikiwa mauzo.
  7. Uwezo wa kufanya kazi kwa shinikizo. Aweze kushughulikia changamoto za mauzo bila kukata tamaa. Awe na ustahimilivu wa kushughulika na wateja wagumu.
  8. Ujuzi wa matumizi ya teknolojia. Awe na uelewa wa matumizi ya kompyuta, program za mauzo, na mitandao ya kijamii ( kama inahitajika). Awe na uwezo wa kutumia CRM (customer relationship management) ikiwa biashara inatumia.
  9. Ubunifu na uwezo wa kutatua matatizo. Aweze kubuni mbinu mpya za kuvutia wateja. Awe na uwezo wa kushughulikia malalamiko ya wateja kwa njia chanya.
  10. Uaminifu na nidhamu. Awe mwaminifu kwa biashara yako na awe na maadili mazuri ya kazi. Awe na nidhamu ya kufuata maelekezo na kufanikisha malengo ya mauzo.

Kwa kuzingatia sifa hizi utaweza kupata mtu sahihi wa kufanya mauzo na kuweza kushawishi wateja kukamilisha mauzo.

Rafiki yako,

Maureen Kemei.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *