Rafiki karibu kitabu hiki kinatoa mwongozo wa kipekee wa kifedha kwa mtu yeyote anayetaka kupata uhuru wa kifedha mapema, kabla hata ya wazazi wao kustaafu.
Hapa kuna mambo makuu ya kujifunza kutoka kitabu hiki:
- Uhuru wa kifedha unaanza na mtazamo sahihi. Badala ya kulenga ‘kuwa tajiri’ lenga kuwa uhuru wa kifedha. Huru kifedha una uhuru wa kuchagua namna unavyoishi bila kutegemea mshahara wa kila mwezi.
- Kiasi unachoweka akiba ni muhimu kuliko mapato. Usisuburi kuwa na kipato kikubwa ndipo uanze kuwekeza. Fanya akiba kuwa kipaumbele hata 1% ya mapato yako ni mwanzo nzuri. Malengo weka 10% , kisha polepole ongeza hadi 20-30% au zaidi.
- Weka bajeti ya maisha inayoakisi vipaumbele vyako. Tumia pesa kwenye vitu vinavyokuletea furaha ya kweli, sio tu fahari. Epuka deni la matumizi kama mikopo ya kadi ya mkopo. Bajeti sio kizuizi, bali ni chombo cha uhuru.
- Muda na riba ya mchanganyiko ( compound interest). Kuanzisha uwekezaji mapema kuna faida kubwa, muda ni rafiki yako.
- Epuka mitego ya kifedha ya kawaida. Kuishi kwa ‘status’ au mashindano na wengine. Kuchelewesha uwekezaji kwa sababu ya hofu au kutokujua. Kuwa na malengo bila mpango wa utekelezaji.
- Fanya uwekezaji rahisi na thabiti. Hakuna haja ya kuwa na akili ya wall street. Hakikisha unaelewa unachowekeza, usiweke pesa mahali kwa sababu tu watu wanasema.
- Hatua ndogo ndogo, matokeo makubwa. Anza leo, hata kama ni kwa kiwango kidogo. Shinda tabia mbaya kifedha kidogo kidogo. Weka mfumo wa kufuatilia maendeleo net worth tracker.
- Uhuru wa kifedha siyo mwisho, ni njia ya maisha. Lengo si tu kuacha kazi mapema, bali kuwa na uhuru wa kuchagua maisha unayotaka. Unaweza kuendelea kufanya kazi unayopenda, bila kulazimishwa na fedha.
Chukua hatua. Uhuru wa kifedha si kwa matajiri tu, ni kwa mtu yeyote aliye tayari kuchukua hatua ndogo leo kwa ajili ya maisha makubwa kesho.
Kipato chako sio kizuizi, bali maamuzi yako ya kila siku ndiyo yanayoamua hatima yako.
Tunakumbushwa kuwa mafanikio ya kifedha si swala la kuwa na pesa nyingi mwanzoni, bali ni juu ya tabia, nidhamu, na kujitolea kwa muda mrefu.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.