Rafiki yangu mpendwa karibu tujifunze kuhusu maisha na mafanikio kutoka kitabu hiki kizuri.
- Usikosee wito wako. Fanya kile ambacho umeumbwa kufanya kile unafurahia kufanya kwa sababu ni wito wako.
- Chagua eneo sahihi. Chagua eneo ambalo ukiwa unafanya jukumu lako haivurugi sana mambo yako.
- Epuka madeni. Madeni yanaturudisha nyuma. Epuka sana kuingia kwenye madeni kwa sababu utakuwa mtumwa wa kulipa madeni kila wakati.
- Kuwa mvumilivu. Huwezi kufanikiwa kwenye maisha kama huna uvumilivu. Kuna wengi ambao wameanzia chini sana wakavumilia hadi wamepata mafanikio.
- Fanya kwa nguvu zako zote. Fanya kazi kwa bidii kwa nguvu zako zote. Kazi ndiye rafiki wa kweli, atakufikisha mbali na kukukutanisha na watu wengi zaidi.
- Usitegemee juhudi zako binafsi. Huwezi kufanikisha kila kitu peke yako, hata wengine wana mchango.
- Tumia dhana Bora. Chagua dhana bora zitakazokusaidia kufikia mafanikio unayoyataka. Jifunze kutumia mashine mbalimbali zitakazokusaidia kurahisisha kazi yako.
- Usiende juu ya biashara yako. Usiishi nje ya kipato chako, watu huwa wanapenda kuanzia juu, wengi hawapendi kuanzia chini. Mara nyingi anzia kwenye level ya kawaida.
- Jifunze kitu chenye manufaa. Ukiwa na ujuzi fulani utaweza kuendesha maisha yako. Kuna msemi unaosema ‘mwenye ujuzi halali njaa.’
- Ongozwa na matumaini lakini usiwe na haraka na uhakika wa kupitiliza. Usihesanu kuku kabla mayai hayajaanguliwa.
- Usitawanye nguvu zako zote.Ukiweza kufanya kitu kimoja kwa muda mrefu utaweza kufanya makubwa, yaani unakuwa bora kabisa unapofanya kitu kimoja. Chagua eneo moja kuu na ufanye bila kuacha.
- Kuwa na utaratibu katika kile unakifanya. Panga utaratibu wa kufuatwa, unapunguza makosa wa kujirudia mara kwa mara.
- Soma magazeti au vitu mbalimbali . Kuwa tayari kujifunza kuhusu biashara, maendeleo binafsi na uchumi. Ili kuwa na uelewa wa kile kinachoendelea.
- Kuwa makini na kazi za nje. Wale wanaokuzunguka ndio wanaokupoteza zaidi. Epuka ushauri ya watu huku nje kwa sababu hajui kwamba wewe unafanya kazi ya wito wako.
- Usimthamini mtu bila amana. Usimwamini mtu au kumpa nafasi ya kipekee bila kujiridhisha kuwa anastahili, kupitia matendo,tabia au historia yake.
- Tangaza biashara yako. Iweze kuwafikia watu wengi zaidi na wajue uwepo wako.
- Kuwa mpole na mkarimu kwa wateja na watu wako wa karibu. Ni sababu moja ya mtu kukukumbuka kuwa umemtoa katika nyakati ngumu.
- Toa msaada. Kwa wenye uhitaji lakini pia kuwa makini kwa wale wale unaowasaidia. Kutoa msaada unakusadia pia.
- Usiwe mpayukaji. Chochote kinachotokea kwenye maisha yako, unapaswa kuwa na utulivu kidogo. Ukimya ni silaha ya mafanikio. Usiwaambie watu kile unachotaka kufanya kabla hajafanya
- Tunza uadilifu wako. Watu wakisha jua wewe sio mwadilifu tena hawataweza kukuamini tena.
Chukua hatua, kwa kufanyia kazi mambo 20 utaweza kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako na kupata mafanikio unayoyataka kwenye maisha yako.
Rafiki yako,
Maureen Kemei .