Mambo 10 Ya Kujifunza Kutoka Kitabu Cha Sales Like Crazy By Sabri Suby.

Rafiki yangu mpendwa kitabu hiki ni mwongozo wenye nguvu kwa mtu yeyote anayetaka kuongeza mauzo kwa njia ya mtandao.

Kinafundisha mbinu halisi za uuzaji wa kijidali zinazoweza kutumika mara moja.

Hapa kuna mambo kumi ya kujifunza na kufanyia kazi.

  1. Toa thamani kwanza ( value first). Usianze kuuza moja kwa moja. Toa kitu cha bure chenye msaada, kama ebook, video au kozi, ili kuvutia na kuvuta imani ya wateja.
  2. Elewa wateja wako vizuri. Fahamu matatizo yao, na lugha wanayotumia. Hii itasaidia kuwasiliana kwa njia inayogusa hisia zao.
  3. Tengeneza ofa isiyozuilika (irresistible offer). Ofa yako inapaswa kuwa na thamani kubwa kiasi kwamba mteja hawezi kusema ‘hapana.’
  4. Tumia mfumo wa mauzo ( sales funnel). Anzisha mahusiano na mteja hatua kwa hatua , kutoka kupata taarifa zao, hadi kuwafanya wanunue mara ya kwanza, hadi kuwa wateja wa kudumu.
  5. Onyesha uthibitisho wa kijamii ( social proof). Weka ushuhuda kutoka kwa wateja waliopita, matokeo waliopata, na idadi ya watu wanaonufaika.
  6. Weka udharura ( Urgency) na Uhaba (Scarcity). Toa ofa kwa muda maalum au kwa idadi ndogo ili kuhimiza watu kuchukua hatua haraka.
  7. Tangaza kwa makini. (Targeted Ads). Tumia matangazo ya kulenga ( Facebook, google n.k) kuwafikia watu wanaohitaji kile unachotoa, sio kila mtu.
  8. Andika matangazo yenye nguvu ( compelling copywriting). Matangazo yako yawe na kichwa kinachovutia, suluhisho kwa shida ya mteja, na wito wa kuchukua hatua ( call to action).
  9. Pima na boresha ( track and optimize). Pima kila kitu, matangazo, email,faneli, na ubadilishe kile kisichofanya kazi. Takwimu ni mwongozo wako
  10. Kuwa Na mfumo, sio bahati. Badala ya kutegemea ‘bahati ‘ kupata wateja, jenga mfumo wa kila siku unaoleta wateja wapya kwa kuuza kwa ufanisi.

Chukua hatua, kwa kuzingatia mambo haya kumi na kufanyia kazi utaweza kupata wateja tarajiwa, kufanya mauzo na kugeuza hao wateja tarajiwa kuwa wateja kamili.

Rafiki yako,

Maureen Kemei.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *