Rafiki yangu mpendwa zifuatazo njia za kuongeza kasi ya usomaji.
Njia ya kwanza ni kusoma kwa kutumia kidole. Fuatisha kidole kwenye sentensi unayosoma na utaweza kusoma kwa kasi kubwa zaidi huku umakini wako ukiwa kwenye ukurasa unaosoma.
Usitamke maneno unayosoma soma kama unaangalia picha na siyo kutamka neno moja moja. Chukua maneno kwa pamoja badala ya neno moja moja.
Tatu; tanua wigo wako wa kuangalia. Badala ya kuzungusha macho kwenye ukurasa unaosoma, tanua wigo wako wa kuangalia ili uweze kuona sehemu kubwa ya ukurasa na kuchukua maneno mengi kwa pamoja.
Nne; jipe zoezi la kusoma haraka kuliko ulivyozoea, hilo litaupa ubongo wako mazoezi na kuweza kusoma kwa haraka zaidi.
Tano; hesabu wakati unasoma, hiyo itaondoa mazoea yako ya kutamka maneno unayosoma na hivyo kuweza kusoma kwa kasi zaidi.
Kuchukua hatua; kila siku tenga dakika 10 za kusoma kwa kasi na chukua hatua ulizojifunza hapa.
Kwa kurudia hatua hizo kwa muda mrefu, usomaji wa kasi utakuwa kitu cha kawaida kwako, utaweza kusoma vitabu vingi, utakuwa na umakini mkubwa na pia utaelewa vizuri yale unayojifunza.
Akupendaye sana,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.