Njia 3 za kuondokana na usumbufu.

Rafiki yangu mpendwa usumbufu ndiye adui mkubwa wa umakini. Usumbufu unaoanzia ndani yako unakuzuia usiwe na umakini kwenye kile unachofanya.

Hapa kuna njia tatu za kuondokana na usumbufu ili uweze kuwa na umakini mkubwa.

Moja ni kufanya zoezi la kupumua. Kwa kupumua kwa umakini mkubwa, inasaidia akili yako kutoka kwenye usumbufu.

Mbili ni kufanya kile kinachokupa wasiwasi. Mara nyingi huwa kuna kitu kinatupa wasiwasi na hivyo kukifikiria kwa muda mrefu. Kitu hicho kinaendelea kuwa usumbufu kwako na kukosesha umakini.

Chukua hatua kwenye kile kinachokupa wasiwasi, Ili ukiondoe kwenye fikra zako. Kwa kufanya kitu au kukipangilia kwa namna ambayo inaondoa wasiwasi inakupa utulivu mkubwa wa kifikra.

Tatu ni kutenga muda wa usumbufu. Kuna vitu ni lazima uvifanye, kama kuwasiliana na kujibu jumbe na barua pepe za watu mbalimbali.

Badala ya kuruhusu hilo kufanyika kila wakati, tenga muda ambao utafanya hayo. Kwa kujua muda fulani ndiyo utahangaika na usumbufu wote, utaweka umakini wako kwenye kile unachofanya na kuepuka usumbufu.

Kuchukua hatua; rafiki yangu jijengee umakini mkubwa wa kiakili kwa kuweza kuituliza kwenye kile unachofanya na hilo litakuwezesha kuwa na fokasi ya kuweza kufanya makubwa.

Akupendaye sana,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *