Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini mabadiliko siyo rahisi, kuvunja mazoea ambayo tayari yapo ni kitu kigumu sana kwa watu.
Hivyo kama unataka mabadiliko yatokee, lazima uyatake kweli. Lazima uwe umedhamiria kweli kubadilika na kuwa tayari kufanya kila kinachohitajika ili uweze kuweza kubadilika.
Kwenye hii dunia, hakuna chochote unachokitaka kweli ambacho utakikosa. Kama kuna kitu unakosa au unashindwa, ni kwa sababu hujakitaka kweli. Kwa sababu hujajitoa kweli kuhakikisha unakipata.
Kabla hujafanya maamuzi, kwenye maisha chochote kile ambacho mtu unakitaka kweli, ambacho haupo tayari kukikosa na upo tayari kufanya kila namna kukipata, lazima utakipata. Hivyo ndivyo kanuni ya asili ilivyo.
Hivyo inapokuja kwenye afya na mengine yote, jiulize ni kwa kiasi gani unataka kubadilika. Kama umedhamiria na kujitoa kweli, hakuna kitakachoweza kuzuia.
Kuchukua hatua; kwa chochote kile unachokitaka kwenye maisha yako, jiulize umedhamiria na unajitoa kiasi gani kuhakikisha unakipata. Kama unaweza kuruhusu chochote kiwe kikwazo kwako, maana yake hujakitaka kweli kitu hicho na hutakipata.
Kitu kimoja zaidi ni kujitoa kisawa sawa kuhakikisha unapata unachotaka na usiruhusu chochote kuwa kikwazo kwako.
Akupendaye sana,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.