Namna ya kudhibiti fikra zako.

Rafiki yangu mpendwa watu wengi hudhani hawawezi kudhibiti fikra zao. Lakini hilo siyo kweli, kudhibiti akili na fikra ni kitu kinachowezekana kabisa.

Na kwa kuwa akili zetu ndiyo zinatupa kila kitu kwenye maisha yetu, udhibiti wake ni hatua muhimu ambayo kila mtu anapaswa kuifanyia kazi.

Kudhibiti akili na fikra ni kitu ambacho kimekuwa kinafundishwa tangu enzi na enzi, kuonyesha ni jinsi gani jambo hilo lina umuhimu mkubwa.

Watu wengi wanalalamika kwamba hawawezi kuweka umakini wao kwenye kitu kimoja. Lakini ukweli ni kwamba nguvu iyo ipo kwa kila mmoja, kinachohitajika ni kuendeleza.

Kudhibiti fikra ni hatua muhimu kwenye kudhibiti maisha. Bila ya kudhibiti akili hakuna kingine kikubwa kitakachowezekana. Na kutokana na umuhimu huo, zoezi la kwanza kwenye siku linapaswa kuwa kudhibiti akili.

Huwa tunaweka juhudi kubwa kwenye kutunza miili yetu, kuanzia kuilisha, kusafisha na kuivalisha. Lakini hakuna juhudi tunaweka kwenye akili, ambayo ni muhimu sana.

Hivyo basi, ule muda wa asubuhi ambao unatoka nyumbani kwenda kwenye shughuli zako ndio unapaswa kuutumia kufanya zoezi la kudhibiti akili.

Kazi yako ni kuhakikisha mawazo yako yanakaa kwenye kitu kimoja ulichochagua. Yatahama mara kwa mara, lakini yarudishe kwenye kile ulichochagua.

Kama unajiambia akili yako haiwezi kuweka umakini kwenye kitu kimoja, kumbuka siku ulipewa jukumu kubwa na linalohitajika haraka.

Akili yako ilitulia kwenye jambo hilo bila kuhama. Hicho ni kiashiria kwamba huo uwezo unao, ni wewe kuufanya kazi kwa makusudi ili kuimarisha umakini wako.

Kuchukua hatua kwa namna yoyote ile usiache tu akili yako izurure hovyo, badala yake idhibiti kwa kuweka mawazo yako kwenye kitu kimoja kwa muda mrefu.

Rafiki yako,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *