Kitu pekee kinachodhihirisha thamani yetu.

Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini kitu pekee kinachodhihirisha thamani ni kuchukua hatua ya kufanya kuliko kuongea (yaani matendo na siyo maneno).

Unaweza kusema utakavyo, lakini watu wataamini zaidi kile unachofanya. Maneno ni rahisi, kila mtu anaweza kusema atakavyo. Lakini matendo ni magumu na hayo ndiyo yanayothihirisha kweli mtu anasimamia wapi.

Utajiskiaje kama kweli kitu ni muhimu kwako, alafu usikifanye, na ni kitu hicho unajua kabisa kuwa kingeleta mafanikio kwako? Lazima utajisikia vibaya, sio.

Lazima utakifanya kwa sababu hutaishia tu kusema. Kama unataka kitu kweli utafanya kila namna mpaka ukipate, hautakubali kuzuiwa na chochote. Hivyo, angalia yale unayofanya, hayo ndiyo yanaonyesha kuwa unajali zaidi.

Na hata kwa wengine, usisikilize wanasema nini, wewe angalia wanafanya nini. Kama maneno na matendo ya mtu vinatofautiana, amini zaidi matendo kuliko maneno.

Hivyo kitu kimoja zaidi ni kwa wale ambao kila mwaka wanasema wanataka kuanza biashara ila hawana mtaji, au uwezo, au muda au kingine chochote, jibu unalo hapo, hawataki kuanza biashara. Wengekuwa wanataka kweli wangeshaanza.

Kuchukua hatua; kinachofuata baada ya hapa ni kufanya maamuzi ya kufanya zaidi kuliko kuongea zaidi.

Rafiki yako.

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *