Rafiki yangu mpendwa watu wengi hudhani kujibu haraka ni kuonekana una akili zaidi.
Yaani kwamba mtu anayechukua muda wa kufikiri kwa kina kabla hajajibu basi ni mjinga au hajui.
Sina uhakika kama itakufaa, lakini Derek kwenye kitabu chake cha ‘hell yeah or no’ anatuambia yeye ni mtu wa kufikiri kwa taratibu na huwa hakimbilii kujibu kitu chochote.
Huwa anajipa muda kwanza wa kukifikiri kwa kina na kujifunza kwa undani ndiyo aweze kujibu.
Anasema watu wanamuona ni mjinga kwa hilo, lakini inamsaidia kwa mengi. Linamwepusha na mabishano yasiyo na tija, lakini pia linamsaidia kujifunza vitu kwa kina.
Habari njema ni kwamba kufikiri kwa kina kunakusaidia uepuke kujibu haraka pale unapoulizwa chochote.
Utajiskiaje kama utakuwa unajipa muda wa kufikiri na kutafakari kwa kina kabla hujajibu mtu yeyote yule? Labda utajisikia vibaya lakini utakuwa umejipa muda wa kuangalia jambo kwa kina, hivyo basi kuepuka mabishano yasiyo na tija.
Kitendo tu cha kujipa muda kitakuepusha na mengi yasiyo na umuhimu kwenye maisha yako.
Rafiki yangu majibu mengi unayoyatoa kwa haraka huwa siyo sahihi, hata kama ni kitu ulichozoea, yanaweza kuwa na mabadiliko ambayo yalishatokea.
Hatua ya kuchukua; unapaswa kujipa muda kabla hujakimbilia kujibu chochote.
Na kama mtu anasisitiza ujibu haraka, jibu lako linapaswa kuwa sijui, au tutaona. Usiwe na wasiwasi maana hakuna ubaya wowote kwenye kutokujua.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.