Njia 2 ya kusema hapana.

Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini zipo njia mbili za kutusaidia kuepuka kushawishiwa vibaya na kufuata mkumbo.

Njia ya kwanza ni kukagua uhalisia wa kundi unaloshawishiwa kulifuata. Badala ya kujiunga tu na kundi, angalia kama kweli kundi hilo lipo na kama lipo jua kama kila mtu kwenye kundi hufuata wengine kwa sababu tu ya wingi wao.

Hili litasaidia kuondoa ile hali ya kufuata mkumbo kwa sababu wengi wanafanya, itatusaidia kujua nini kimewafanya wengi hao wafanye hivyo.

Njia hii ya kwanza nzuri kutumia pale unapojikuta njia panda au ukiwa na hali ya kutokuwa na uhakika. Badala ya kujiunga tu na kundi, jua kundi hilo linasimamia nini.

Njia ya pili ni kujiepusha na ujinga wa kundi, pale unapoona kuna jambo halipo sawa, badala ya kujiambia kuna mwingine ameshachukua hatua. Jua kila mtu anafikiria mwingine ameshachukua hatua na hivyo hakuna anayechukua hatua.

Wewe vunja hilo kwa kuwa mtu anayechukua hatua na hata kama mwingine ameshachukua, hakuna unachokuwa umepoteza.

Wengi wanaodhurika kwa kufuata mkumbo, kama waliojua kwa kushawishiwa na viongozi wa kidini ni kwa sababu wanakuwa hawapati muda wa kufikiri mwenyewe nje ya kundi wanalokuwepo.

Kwa kuwa kila anayewazunguka anafanya, wanaona ndiyo kitu sahihi kufanya. Lakini wewe ukiwa mtu wa kukaa nje ya kundi kidogo na kufikiri kwa akili yako, utaona jinsi yale yanayofanyika yasivyokuwa sahihi.

Chukua hatua; rafiki yangu kwenye maisha tunapaswa kujifunza kusema hapana na kukataa kufuata kundi. Hapo tutaweza kujipa muda wa kufikiri na kufanya maamuzi sahihi.

Mwandishi wako,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *