Maamuzi makubwa 3 yakufanya kwenye maisha yako.

Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini kuna maamuzi makubwa matatu unayoyafanya kwenye maisha yako, eneo unaloishi, watu unaishi nao na kile unachofanya.

Haya ni maamuzi ambayo yataathiri sana maisha yako, lakini wengi hawayapi uzito unaostahili. Wengi huyafanya kwa mkumbo na siyo kufikiria wapi wanataka kufika kisha kufanya maamuzi hayo kwa mwongozo huo.

Eneo unalochagua kuishi utakaa kwa muda mrefu na itakuwa na athari chanya au hasi kwenye mafanikio yako, hivyo lichague kwa umakini.

Mahusiano yako na wengine yana ushawishi mkubwa kwenye kile unachofanya, hivyo chagua vizuri wale unaokwenda kujihusisha nao kwenye maisha yako.

Kadhalika kazi au biashara unayokwenda kufanya, itachukua sehemu kubwa ya maisha yako na inahusika sana kwenye mafanikio yako, hivyo chagua kwa umakini nini unakwenda kufanya.

Katika kufanya maamuzi hayo matatu, hakikisha yanatoka ndani yako na siyo unayafanya kwa kufuata mkumbo.

Mwandishi wako,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *