Katika zama tunazoishi sasa zama zenye kelele na usumbufu wa kila aina, kupata utulivu wa akili ni kitu kigumu sana.
Rafiki sina uhakika kama itakufaa, lakini iyo ni kwa sababu kila mtu anawinda umakini wako na kutaka kuteka akili yako.
Hivyo basi, kupata utulivu wa akili lazima uzuie kelele na usumbufu visiingie kabisa kwenye akili yako.
Unaweza kufanya hivyo kwa kuzingatia haya:
- Usifuatilie habari kwenye tv,redio,magazeti au mitandaoni.
- Ondoka kwenye mitandao ya kijamii.
- Usibishane na mambo ya siasa,michezo, dini au mapenzi.
- Usihangaike kufuatilia maisha ya watu maarufu.
Unaweza kujiuliza utajuaje yale yanayoendelea kama hufuatilii habari. Kwanza mengi yanayoendelea kwenye habari kila siku siyo muhimu. Na yale muhimu kabisa lazima yatakufikia kupitia watu wengine.
Njia bora ya kutumia akili yako ni kujifunza kupitia usomaji wa vitabu na makala zenye maarifa yenye tija na unayoweza kutumia kupiga hatua.
Chuka hatua; rafiki unapaswa kujua kwamba habari zinazoenezwa ni hasi na za kusisimua, achana nayo.
Rafiki wako,
Maureen Kemei .
kemeimaureen7@gmail.com.