Ya Kwanza ni kichocheo, huchukua taarifa kwenye akili kuhusu tabia fulani. Ni taarifa ambazo akili inapata. Kinaweza kupitia kwa kuona, kusikia, kunusa au kuhisi.
Kubadili, sheria ya Kwanza FANYA TABIA KUWA WAZI.
Njia ya kufanya tabia iwe wazi ni
1.kuwa na ubao ambao unaandika kile ambacho unataka kufanyia kazi, unapoandika na kuona kile ulichoandika ni rahisi kufanyia kazi.
2. Kuweka Nia ya kufanya kitu kama kwa maandishi kuwa katika hali fulani nitafanya kitu fulani.
3. Kuweka tabia mpya kwenye tabia ya zamani.
4. Kuboresha mazingira na kuandaa na tabia unayotaka kujenga.
5. Kuitenga eneo maalum la kufanya tabia fulani kama kusoma au kuandika.
Kuvunja, WEKA KIFICHONI. Kama Kuna tabia unatamani kubadilisha kifiche, kama kuacha kuzurura mtandaoni bila kufanya kitu yenye tija kafiche simu.
Hatua ya pili ni TAMAA.tamaa inaleta hamasa ya kuchukua hatua fulani ili uweze kupata matokeo unayotarajia.
Sheria y pili,KUJENGA, IFANYE IVUTIE.tamaa inatokana na ubongo kupata kemikali ya dopamine ambayo Inamfanya mtu ajiskie vizuri.
Baadhi ya njia za kufanya ziwe za kuvutia ni hizi.(i) Iweke tabia unayojenga na tabia nyingine ambayo tayari unapenda kufanya. Tanguliza kufanya tabia mpya kabla ya tabia uliyozoea.
(ii) zungukwa na watu ambao nao wanafanya tabia ile unayotaka kujijengea. Sisi binadamu ni viumbe vya jamii, huwa tunaiga yale ambayo wengine wanafanya.
(iii). Chagua mtu sahihi ya mfano kwako anayefanya au alikuwa anafanya tabia iyo unayojifunza.
(iv). Ihusishe tabia unayojenga na matokeo chanya.
Kuvunja, IFANYE ISIYOVUTIA. Kubadili mtazamo juu ya tabia hiyo. Orodhesha hasara ya tabia iyo.
Hatua ya tatu. KUCHUKUA HATUA. sheria ya tatu, kujenga, IFANYE TABIA KUWA RAHISI KUFANYA. Igawe tabia kwenye hatua ndogo ndogo ambazo unazoweza kufanya bila ugumu wowote. Kadri unavyorudia ndivyo tabia inavyojengeka kwenye akili.
Yafuatayo ni mambo ya kufanya tabia kuwa rahisi.
(I). Ondoa msuguano au ukinzani, hakikisha uhitaji nguvu nyingi kufanya tabia husika.
(ii).tengeneza mazingira kuwa rahisi, kama kusikiliza audio za vitabu wakati unafanya mazoezi.
(iii) tumia sheria ya dakika mbili, jiambie kama nafanya kwa dakika mbili tu, ukishaanza ni rahisi Kuendelea.
(iv). Tengeneza mazingira ya kuvunja tabia kuwa kugumu kwako kuliko Kuendelea. Kwa mfano,kama umekuwa unajiambia utaanza biashara lakini huanzi,lipia kabisa eneo la biashara, hivyo litakusukuma kuanza. Kwa sababu usipoanza fedha zitapotea.
Kuvunja, IFANYE KUWA NGUMU. Tabia unazotaka kuzivunja, niweke ugumu katika kuzifanya.
Hatua ya nne. ZAWADI.
Lengo kuu la kuchukua hatua ni kupata zawadi. Zawadi inaturidhisha kwa kutuliza tamaa na kutufundisha kwa kuweka Kumbukumbu kwenye akili kwamba kama nataka kupata zawadi fulani basi nichukue hatua sahihi.
Sheria ya nne. IFANYE TABIA YENYE KURIDHISHA.kujenga, IFANYE YA KURIDHISHA. Iwe inakupa msukumo wa kuirudia tena kwa kufanya yafuatayo.
(I). Ifanye zawadi kuwa ya haraka, fanya matokeo kuwa ya haraka litakusukuma kufanya zaidi.
(ii). Jipe mda kila unapokamilisha kufanya tabia mpya unayotaka kujenga, kwa kupata zawadi, unasukumwa kufanya zaidi.
(iii). Kuwa na njia ya kufuatilia maendeleo yako ya kila siku, weka alama kwenye calenda, kadiri alama zinavyokua, lengo lako linakua kutovunja minyonyororo. Hivyo, utaendea ndivyo usiharibu maendeleo yako.
(iv). Tumia sheria ya kutokukosa mara mbili, unapokutana na dharura, usikose mara mbili.
5. Kuwa na mtu unayeshirikiana naye kwenye kujenga tabia, iwapo mtu uyo hatakuwepo hutataka kumwangusha bali utaendelea kufanya.
Kuvunja, IFANYE ISIYORIDHISHA. Unafanya kwa kutumia hatua mbili
Ya Kwanza, kutafuta mtu unayemheshimu, kisha kumwomba akusimamie kwenye kuvunja tabia hiyo. Unamwahidi kwamba hutafanya tabia hiyo na kuweka wazi. Hatua hizo zinapaswa ziwe zinakuumiza kiasi kwamba ukifikiria kufanya unakosa kabisa msukumo.
Ya pili, kuweka mkataba hadharani ya kuvunja tabia iyo na kuweka gharama au adabu kali pale ambapo utarudi kwenye tabia iyo.
Ndugu yangu hayo ndiyo nmekuwa nikijifunza kutoka katika kitabu cha kanuni ya mafanikio. Nmeanza kufanyia kazi na ninaona matokeo, kitu kizuri ni Kuendelea kufanya kila siku bila kukoma.
Asante Sana kwa kuchukua muda wako makini sana na kuyasoma makala haya. Anayekuleta makala haya ni mimi wako mwaminifu na mwanafunzi Maureen Kemei.