Rafiki yangu mpendwa kabla hujafanya maamuzi, unaweza kusema utakavyo, lakini watu wataamini zaidi kile unachofanya kuliko unachoongea.
Maneno ni rahisi kila mtu anaweza kusema atakavyo, lakini matendo ni magumu na hayo na ndiyo yanadhihirisha kweli mtu anasimama wapi.
Kama kweli kitu ni muhimu kwako utakifanya, hutaishia tu kusema. Kama unakitaka kitu kweli utakifanya kila namna mpaka ukipate, hautakubali kuzuiwa na chochote. Hivyo angalia yake unayofanya hayo ndiyo yanaonyesha nini unajali zaidi.
Na hata kwa wengine, usisikilize wanasema nini, wewe angalia wanafanya nini. Kama maneno na matendo ya mtu vinatofautiana, amini zaidi matendo kuliko maneno.
Hivyo kwa wale ambao kila mwaka wanasema wanataka kuanza biashara ila hawana mataji, au wazo, au muda au kingine chochote, jibu unalo hapa hawataki kuanza biashara. Wangekuwa wanataka kweli wangeshaanza.
Sina uhakika kama itakufaa, lakini ili thamini yetu idhihirike kwa watu ni kwa kuweka matendo zaidi kuliko maneno.
Rafiki wako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.