Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini ndani yako kabisa unajua nini ambacho unataka kwenye maisha yako.
Kuna sauti inayokuambia nini unapaswa kufanya na hata ukiipuuza sauti hiyo, bado haiondoki. Kuna mambo ukiyaona huwezi kuyavumilia, ungependa yawe bora zaidi.
Huu ndiyo wakati wa wewe kuwa wewe na kuacha kupoteza muda wako na maisha yako kwa mambo yasiyo kuwa na tija kwako
Fanya zaidi ya ulivyozoea maana ndiyo njia ya kuweza kufanya makubwa zaidi. Kumbuka hamasa na msukumo uliokuwa nao tangu utotoni na uamshe tena ndani yako sasa. Hayo hayakuondoka, ila tu uliyazima, unaweza kuyawasha tena sasa.
Pima ushindi wako kwa hatua unazopiga na siyo kwa vitu unavyokuwa navyo au unavyowazidi wengine.
Chukua hatua; ongoza hata kama huna cheo, shawishi hata kama huna nafasi na fanya kazi kwa viwango vya juu sana na utaweza kufanya makubwa.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.