Maadili 13 Ya Benjamin Franklin.

Rafiki yangu mpendwa bila shaka leo tunajifunza maadili 13 aliyochagua kuyaishi na kujipima nayo. Marafiki mambo hayo ni kama yafuatayo;

  1. Ujasiri. Kuwa makini kwenye vyakula na vinywaji.
  2. Ukimya. Kuepuka mazungumzo yasiyo na maana na kuepuka kutumia maneno machafu.
  3. Mpangilio. Kila kitu kifanyike kwa mpangilio mzuri.
  4. Maamuzi. Fanya ulichoahidi bila kuhairisha.
  5. Ubahili. Kuwa makini na matumizi yako na epuka ubotevu.
  6. Kazi. Tumia muda wako vizuri na epuka kufanya mambo yasiyo na umuhimu.
  7. Ukweli. Usidanganye yeyote na kuwa mkweli kwako mara zote.
  8. Haki. Watendee watu kwa usawa na mara zote fanya kilicho sahihi.
  9. Kiasi. Epuka kuzidisha chochote kile, kiwe kizuri au kibaya.
  10. Usafi. Uweke mwili wako, makazi yako na mazingira yako kwenye hali ya usafi.
  11. Utulivu. Kuwa na amani ya ndani na usisumbuke na vitu vidogo vidogo.
  12. Uadilifu. Usijihusishe na zinaa.
  13. Unyenyekevu. Waige wale waliofanya makubwa hapa duniani.

Ili kuhakiksha anayaishi maadili hata 13, Franklin alichagua kuyageuza kuwa tabia kwake. Maana tabia Ina nguvu kuliko kipaji au maamuzi.

Alitengeneza chati ya kujipima kila siku na kabla ya kulala alijitathmini jinsi alivyoishi maadili hayo kwenye siku husika.

Rafiki hapa tunajifunza mambo makubwa mawili;

Moja ni kuwa na maadili ambayo mtu unasimamia na kujipima nayo kwenye maisha yako.

Mbili ni kuyageuza maadili hayo kuwa tabia kwa kujifanyia tathmini kila siku na kurekebisha pale unapokosea.

Chukua hatua, rafiki tunapaswa kufanyia kazi maadili hayo ambayo tumejifunza kutoka kwa muuzaji bora kuwahi kutokea Benjamin Franklin.

Rafiki yako,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *