Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini watu wengi wamekuwa wakifanya mambo kwa ajili ya kujijengea sifa baada ya kuondoka hapa duniani.
Wanafanya kwa lengo la kukumbukwa vizazi kwa vizazi kwa majina yao kuandikwa maeneo muhimu au kuchongewa masanamu.
Lakini kama ilivyo kwenye mambo mengine ya maisha, unapolazimisha kitu, huwa hakitokei. Unapofanya mambo ili ukumbukwe, hakuna anayekukumbuka, kwa sababu unakuwa siyo rahisi.
Tunapaswa kuachana na msukumo wa kufanya vitu ili tukumbukwe au kuacha alama. Badala yake, tuchague kuishi maisha halisi, tusimamie kile kweli tunachokiamini na tutakuwa na maisha bora huku pia tukiwa na nafasi kubwa ya kuendelea kukumbukwa.
Watu hawatakukumbuka kwa sababu unataka wakukumbuke, bali watakukumbuka kwa aina ya maisha unayoishi.
Hivyo wajibu wako mkubwa ni kuyaishi maisha yako kwa uhalisia na ukamilifu wake.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.