Rafiki yangu mpendwa mafanikio yetu yanajengwa au kubomolewa na tabia tunazoziishi kila siku.
Ndiyo maana Huwa inasemekana kwamba tunajenga tabia na kisha tabia zinatujenga.
Tabua hayo 5 ni kama yafuatayo;
- Kila siku amka mapema. Ukishaamka usiangalie simu wala usumbufu wowote, bali anza kwa kufanya sala au tahajudi, kisha chukua notebook yako na andika vipaumbele vya siku yako.
- Kila siku fanya mazoezi kwa dakika zisizopungua 30.
- Kila siku soma kitabu kwa angalau dakika 30, chagua kitabu chochote unachotaka kusoma, iwe ni cha maendeleo binafsi au maendeleo ya kitaaluma kisha soma kwa angalau dakika 30 kila siku.
- Kwa siku pangilia na dhibiti ulaji wako, punguza kabisa vyakula vya wanga na sugari, kula mboga mboga na matunda kwa wingi, kula nyama kwa kiasi na kunywa maji mengi. Pia dhibiti sana vilevi unavyotumia.
- Kila siku mpigie simu mtu mmoja wa karibu, ndugu jamaa na marafiki na kuwa na maongezi naye ya kuboresha mahusiano yenu.
Chukua hatua; rafiki yangu ni mambo hayo matano tukifanyia kazi bila kuacha tutaweza kufanya makubwa.
Rafiki Yako,
Maureen Kemei.