Rafiki yang mpendwa Sina uhakika kama itakufaa, lakini msongo wa mawazo ni hali inayotokana na fikra nyingi ngumu za maisha.
Ili kupunguza zingatia hatua zifuatazo:
- Mazoezi. Kufanya mazoezi ya mara kwa mara huchochea utoajj wa endorphins, kemikali zinazoboresha hali ya hewa, huku ikipunguza homoni za msongo kama cortisol. Mazoezi oia husaidia kuboresha usingizi, ambayo ni muhimu kwa kupunguza msongo wa mawazo.
- Kupumua kwa Kina( deep breathing. Kupumua polepole na kwa kina husaidia kupunguza msongo kwa kudhibiti mfumo wa neva ambao una jukumu la kutuliza mwili. Fanya mazoezi ya kuvuta pumzi kwa sekunde tank, kuishikilia kwa sekunde chache, kisha kuachia polepole.
- Maombi ya kushukuru. Maombi haya unamshukuru Mungu kwa mema aliyokutendea, unaweza kuorodhesha kwenye karatasi na kusoma. Hii husaidia kuondoa msongo ya kulalamika na wasiwasi wa baadae, akili yako itatambua kuwa Mungu aliye kutendea haya atakutendea na hilo unalopitia. Maombi ya kushukuru husaidia kupunguza msongo wa mawazo.
- Mtindo wa maisha bora. Kulala kwa muda wa kutosha, kula chakula chenye virutubisho sahihi, na kufanya mazoezi ya mara kwa mara husaidia mwili na akili kuwa na uwezo wa kukabiliana na msongo wa mawazo.. Kuepuka kafeini na sukari nyingi husaidia kudhibiti mihemko na kuepuka mabadiliko ya ghafla ya nguvu za mwili.
Chukja hatua: Rafiki baada ya kugundua ishara za msongo wa mawazo unaweza kujaribu njia hizi na unaweza kupunguza msongo haya.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.