Rafiki yangu mpendwa karibu sana leo tunajifunza misingi nane ya kuzingatia ili kufanikiwa kwenye biashara yoyote ile, mambo haya nimejifunza kutoka kwa kipindi cha ongea na Kocha Dr Makirita Amani.
Mambo haya ni kama yafuatayo ;
- Kuwa na imani yenye nguvu na isiyo yumbishwa. Kama huamini ndani ya nafsi yako kuwa utafanikiwa kwenye biashara yako hivyo, huwezi ukafanikiwa. Kujenga ndani yako imani dhahiri kabisa inakufanya uwe imara kwenye biashara yako.
- Kuwa na mapenzi ya dhati. Watu wengi wanaanza biashara kweli vizuri kabisa lakini wakikosa mapenzi ya kweli na kujitoa kwenye kujenga biashara hiyo hiwezi fanikiwa.
- Chukua hatua kwa haraka. Kama huwezi ukachukua hatua sasa tena kwa haraka huwezi fanikiwa kwenye biashara.
- Kuwa bora zaidi kwenye uimara yako. Kila mmoja wetu ana maeneo yenye uimara na dhaifu, unapaswa kuwa na uimara zaidi kwenye maeneo yako ya uimara.
- lazima kuwa na uerefu na umakini. Lazima uzitumue vizuri rasilimali zako, na siyo kuzitawanya ovyo.
- lazima kutawala sehemu ya soko au (niche) . Usifanye biashara ambayo unashindana na watu. Tafuta biashara au ona kile ambacho watu wanakitaka sana kisha anza kuifanya kwa ubora zaidi.
- Kuwa na mtazamo endelevu kama miaka kumi na kuendelea. Unapaswa kuangalia miaka kumi kutoka sasa utakuwa wapi. Hivyo utaweza kujitoa vilivyo kwa kuweka rasilimali zako kwenye biashara kama muda, fedha, na nguvu zako.
- Kuwa wa tofauti kabisa na wengine kuwa tayari kuonekana kichaa. Namna pekee ya kujenga biashara yako ni kuonekana kichaa au mwendawazimu ili uweze kufanya kubwa kwenye biashara yako. Hufau kukaa kistaraabu au kwa mazoea kama wengine unapaswa kuwa wa tofauti, kufanya kwa tofauti kabisa na wengine. Unaenda kinyume na mazoea yaliyo kwenye jamii.
Chukua hatua ; rafiki tunapaswa kuzingatia mambo hayo nane ili tuweze kufanikiwa kwenye biashara zetu.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
KEMEIMAUREEN7@GMAIL.COM