Rafiki yangu mpendwa karibu sana siku hii njema ya leo nikushirikishe yale nimejifunza kutoka hadithi hii fupi cha mzee anayepambana na bahari katika kipindi ambacho anaonekana hana bahati.
Anafanikiwa kumuua samaki mkubwa, lakini anapitia magumu katika kumpeleka samaki huyo ufukweni. Anatumia kila zana kupambana nguvu, nia na akili.
Yale nimejifunza ni kama yafuatayo ;
- Umuhimu wa kupambana hadi tone la mwisho bila kukata tamaa. Jinsi Santiago pamoja na uzee wake alivyoweza kupambana na japo hakupata alichotaka lakini hakukata tamaa.
- Umuhimu wa kuwa na watu wa kutusaidia, kwani mara nyingi Santiago alitamani kijana angekuwa karibu yake amsaidie.
- Kufanya maamuzi ni kitu kingine tunajifunza, hasa kupitia kijana ambaye alipenda kujifunza kwa mzee, lakini familia yake ikawa kikwazo. Mwisho kabisa anaamua kutokusikiliza familia yake ili aweze kujifunza.
- Umuhimu wa nia na akili katika mapambano yoyote yale, hata kama nguvu zitakuishia, pambana kuvitunza hivyo viwili, kuwa na nia ya dhati na kuhakikisha akili inafikiri sana.
- Haijalishi unapitia nini, lazima uhakikishe unakula ili mwili uwe na nguvu na pia na pia akili inapumzika ili akili iweze kufikiri vizuri.
Chukua hatua; kila mmoja wetu ana mapambano yake, muhimu ni sisi tupambane bila kukata tamaa.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
KEMEIMAUREEN7@GMAIL.COM