Rafi yangu mpendwa uvivu ni tabia ambayo mtu anajijengea tu yeye mwenyewe siyo kwamba anazaliwa nayo. Anajitengenezea bila yeye kujua ya kwamba anajitengenezea tabia ambayo itaua kabisa ndoto zake.
Yafuatayo ni mambo matano ya kuangalia ili kujua kama una tabia hiii.
- Mpangilio wako wa muda kwa siku nzima. Kuanzia kwenye kuamka, mpangilio wa ratiba zako za siku mzima. Watu wenye maono makubwa hufuatilia ratiba zao bila kuacha kufanya yale wanayopanga. Lakini wenye uvivu hawana ratiba yoyote ile, wanaamka saa yoyote tu na kufanya mambo tu bila mipango.
- Utendaji wako wa kazi zako za kila siku siyo wa kuridhisha.
- Hujishulishi kkwa chochote kile ambacho kitakusaidia wewe kufika kwenye ndoto yako, unasubiri misaada.
- Una malalamiko kila kukicha. Utamlalamikia mzazi, serikali, mwajiri au boss,mwenzio au mpenzi, mchumba wako.
- Huwazi cchochote juu ya kesho yako. Hii kwa lugha nyingine mtu anasema bora maisha yaende, maisha ni haya haya tu, hakuna maisha mengine.
Ikiwa uunataka kujikwamua kutoka kwenye tabia hii ya uvivu, anza leo kujijengea tabia ya kufanya mambo yako kwa bidii hata kama ni jambo dogo sana, wewe lifanye kwa bidii, hii litakusaidia sana kufika kwenye mafanikio makubwa.
Kama una ndoto kubwa ifanyie kazi kwa bidii bila kukata tamaa na bila kuangalia ni nani anafurahia au nani hafurarahii ndoto yako.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.