Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini tabia hii ni kama imekuwa sugu sana kwa baadhi ya watu.
Tabia ya kutaka kuonewa onewa huruma ni tabia inayouwa uwezo wa mtu wa ndani nikimaanisha uwezo wa kuwaza mambo kwa ukubwa na upana zaidi.
Uwezo wa kutatua na kutafuta suluhu za changamoto zinajitokeza, uwezo wa kufikiria kesho itakuaje na na mengine yanayofanana nayo.
Njia za kujua una tabia hii ni kama;
- Ukipatwa na tatizo kidogo tu, unataka kila mtu ajue na waanze kulifanyia kazi wao siyo wewe.
- Unakuwa ni mtu wa kukuza jambo, hata kama ni jambo dogo la kawaida tu la kutatulika basi unalikuza na kutaka kila mtu akuonee huruma.
- Unakuwa ni mtu wa kujielezea sana matatizo yako na mapito yako kwa watu kuliko kuelezea ni namna gani unataka kupiga hatua ili uweze kufika kwenye ndoto yako.
- Ukionyeshwa fursa yoyote ile ambayo itakusaidia kupata kipato basi unataka upewe na mtaji.
Tabia ya kuonewa huruma itaua uwezo wako wa kufikiri na kutatua changamoto, na itakuzuia sana kufika kwenye ndoto zako.
Chukua hatua, jikubali kwamba unaweza kufanikiwa kwenye ndoto yako, jikubali kwamba una uwezo mkubwa ndani yako, usijidharau.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.