Rafiki yangu mpendwa kuna msemo unaosena hivi time is money ikiwa na maana kwamba muda ni pesa.
Muda ni moja ya rasilimali kubwa sana kwenye maisha ya mwanadamu katika safari ya kufika kwenye ndoto zako ukilinganisha na rasilimali nyingine, kwa sababu muda ukipita umepita, muda huwa haurudi nyuma ni kama mto ukishuka umeshuka haupandi.
Rasilimali nyingine unaweza kuzitafuta kama fedha au watu na zikapatikana lakini muda siyo kitu cha kutafuta kikishapotea.
Njia ya kujua kwamba una tabia ya matumizi mabaya ya muda.
- Hujali muda kabisa. Muda wako unaweza kutumika tu hovyo bila kujali ni nini kitatokea badala ya muda huo kupotea.
- Kuruhusu kila mtu kutumia muda wako wote. Ni ile ukipigiwa simu na mtu yeyote bila ratiba yeyote basi unafuata chenye anataka yeye ufanye.
- Kushinda kwenye mitandano ya kijamii hasa kwenye page za udaku. Simaanishi mitandao ni mbaya bali matumizi yake yakoje kwako? Huna muda maaalum ya kuingia kwenye mitandao ya kijamii, na hata ukiingia huna kitu maaalum unachokitafuta ili ujifunze kwa siku hiyo.
- Malengo yako na mipango yako hayana muda maalum wa kuyatekeleza.
Tabia hii ukiiendekeza sana utajikuta ni yule kijana ambaye muda wote unajisemea ningejua ningefanya hivi, ningejua nisingewapa watu muda wangu, ningejua muda niliopoteza na watu ningewekeza kwenye biashara.
Unabaki na majuto ndani yako. Njia za kutoka kwenye majuto haya ni kama yafuatayo ;
- Panga siku yako kabla hujaanza.
- Pangilia kila ratiba zako na muda wake.
- Malengo yako ya mwaka mzima yaweke kwenye muda maalum wa kuyatimiza.
- Si kila mtu ni wa kuonana naye kila wakati.
- Punguza matumizi yako ya simu nikimaanisha muda wa kukaa mtandaoni.
Chukua hatua ; rafiki usikubali yeyote yule akaupoteza muda wako iwe ni mtaani, kazini, kwenye biashara zako na kwenye mahuasino yako.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.