Mitazamo 6 Sahihi Kuhusiana Na Utajiri.

Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini kuna mitazamo sahihi ambayo unapaswa kuijenga ili uweze kupata mafanikio na utajiri ambao unaitamani kwenye maisha yako.

Yafuatayo ni njia sita ya kujenga mtazamo sahihi.

  1. Una uwezo mkubwa ndani yako kuliko vile ambapo wewe unautumia. Bado unaitumia asilimia chache zaidi ya uwezo ulio ndani yako.
  2. Utajiri ni haki na wajibu wako wa kimsingi. Unapaswa kukiri mwenyewe kwa mdomo wako kuwa utajiri ni haki yako na ni wajibu wangu kutafuta utajiri huo.
  3. Njia bora ya kuwasaidia maskini ni kutokuwa maskini. Wanaposema tunapaswa kuwasaidia maskini, inatupasa sisi wenyewe tuwe matajiri kwanza ili tuwasaidie maskini.
  4. Kila kitu kinasababishwa, kuna kichochea cha kila kitu, kwa hivyo ili uwe tajiri lazima uchochee kwa kutafuta na ukiwa maskini pia ni wewe umechochea umaskini huo.
  5. Hakuna njia moja pekee ya kujenga utajiri. Yapo njia nyingi halali mno za kujenga utajiri.
  6. Kama wengine wameweza kuwa matajiri na mimi ninaweza kupata utajiri mkubwa. Naamini kabisa ndani yangu kuwa, naweza kuwa tajiri na wewe rafiki unaweza kuwa tajiri.

Chukua hatua; rafiki moja kati ya mafanikio kwenye maisha ni kuwa na mtazamo sahihi juu ya mafanikio yako kwa ujumla. Kwa hivyo basi tunapaswa kuwa na mtazamo sahihi ili tuweze kuijenga utajiri.

Rafiki yako,

Maureen Kemei.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *