Mambo 5 Ya Kujifunza Kutoka Kitabu Cha Don’t Go Back To School

Rafiki yangu mpendwa karibu siku ya leo nikishirikishe mambo 5 nininayo jifunza kutoka kitabu cha don’t go back to school.

Mambo 20 ninayojifunza katika kitabu Cha (Don’t Go Back To School) by Kio Stark ni kama ifuatavyo;

  1. Watu waliofanya machaguo katika kazi zao ndio wale wenye furaha. Mtu ambaye anafanya kazi asiyoipenda anakua hana furaha na kazi yake inamsababisha hali ya kutokuwa hata mbunifu katika KAZI yake na kuleta matokeo ambayo si mazuri. Ubunifu ni chanzo cha furaha kwa hiyo ukikosa furaha ni mbaya katika utendaji wa kazi. Fanya kazi au kitu unachokipenda kitakuletea furaha.
  2. Kuna njia mbili za kupata taarifa nazo ni ; kusoma, kusikiliza. Maarifa yanapatikana katika kusoma vitabu huwezi na maarifa mengi kama wewe siyo mtu wa kujifunza na njia ya kusikiliza, kusikiliza ni bora kuliko kuongea. Mtu anayesikiliza anajifunza zaidi kuliko mtu anayeongea. Jifunze kusikiliza ili kuchota maarifa mengi.
  3. Siku hizi kujifunza sio mpaka uende shule ukasome . Shule unatembea nayo siku hizi ukitaka kujifunza kuhusu kitu fulani unaingia katika mtandao na kujifunza kitu huko. Vitabu viko vingi online ni wewe kushindwa kujifunza tu. Maarifa huwezi kupata shule peke yake.
  4. Kujifunza nje ya shule kama vile kujisomea kitabu inahitaji motisha, hamasa ya kutoka moyoni. Ni injini ya ndani ndio inaweza kuratibu mambo binafsi ya kujifunza. Ukikosa hali ya kupenda kujifunza bila sharti unakua ni mtumwa.
  5. Njia ya kujifunza na kumfundisha mwenzako ni njia nzuri sana ili ukae na maarifa wapatie na wenzako kile ulichojifunza. Njia nzuri ya kujifunza ni kushirikisha wengine uliyojifunza.

Chukia hatua huwezi kuleta sababu tena za kwa nini hujifunzi kwa bidii wakati elimu inapatikana hapo ulipo ni wewe tu kuchukua hatua.

Rafiki yako,

Maureen Kemei.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *