Namna 10 Ya Jinsi Unavyoweza Kushukuru.

Rafiki yangu mpendwa Mwenyezi Mungu (au kwa namna yoyote unavyoitambia nguvu hii kuu) ametupatia baraka nyingi pengine kuliko yale ambayo tumekua tukiyaona kama kero katika maisha yetu.

Hivyo basi, yatupasa kushukuru kwa yale ambayo tayari tumebarikiwanayo kabla ya kudhihirishwa kwa yale ambayo bado yapo tu katika hisia na mapenzi yetu.

Haijalishi uwezo ulionao, popote pale ulipo na kwa namna yoyote uliyonayo, bado unaweza kushukuru kwa namna tofauti.

1️⃣Tafakari kila siku jipatie muda wa kutafakari kila jioni kuhusu mambo mazuri yaliyotokea katika siku yako. Andika mambo matatu unayoshukuru kila siku.

2️⃣Toa sadaka kwa wenye mahitaji tembelea watu wenye mahitaji maalum, kama vile watoto yatima au wagonjwa hospitalini, na wape msaada wa vyakula, mavazi, au hata maneno ya faraja.

3️⃣Shukuru kwa maneno na vitendo wakati mwingine kusema “Asante” kunaweza kuwa na maana kubwa kwa wengine. Pia, jitahidi kuonyesha shukrani zako kwa vitendo kama kuwasaidia wengine bila malipo.

4️⃣Andika ujumbe wa shukraniA andika barua au ujumbe mfupi wa shukrani kwa mtu aliyekusaidia au aliyefanya jambo zuri kwako.

5️⃣Sali au fanya maombi shukuru kwa yale uliyonayo kupitia sala au maombi kwa Mungu au nguvu ya juu unayoiamini.

6️⃣Onyesha ukarimu kwa wengine kuwa mtu wa kutoa msaada, hata kwa vitu vidogo kama tabasamu, msaada kazini, au kuwajulia hali wengine mara kwa mara.

7️⃣Sherehekea/furahia mafanikio ya wengine jifunze kushukuru kwa ajili ya furaha ya watu wengine. Sherehekea mafanikio ya watu wa karibu yako na uwapongeze.

8️⃣Ishi katika hali ya kuridhika jifunze kuwa na moyo wa kuridhika na kile ulicho nacho badala ya kulalamikia unachokosa. Hii itakusaidia kuona mazuri zaidi maishani.

9️⃣Jitolee katika jamii yako jiunge na vikundi vya kujitolea kusaidia jamii yako. Hii si tu kuwasaidia wengine bali pia kukuza moyo wa shukrani.

🔟Jali mazingira na asili tembelea maeneo ya asili, kama misitu au bahari, na ujifunze kushukuru kwa uwapo wa uzuri huu katika dunia.

Chukua hatua rafiki yangu hifadhi mazingira kwa kupanda miti na epuka uchafuzi.

Rafiki yako,

Maureen Kemei.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *