Hatua 5 Za Kutoka Kwenye Madeni.

Rafiki yangu mpendwa 99% ya watu wengi wamo kwenye madeni mabaya. Lakini hatua za kujitoa kwenye madeni mabaya kunahitaji kazi unapaswa kuweka utaratibu wa kuanza kulipa.

Hapa kuna hatua 5 Za kujikwamua kwenye haya madeni mabaya. Ni kama yafuatayo;

  1. Kujua kiasi gani cha deni unalodaiwa. Unakuwa na mahali pa kuanzia na unaanza kulipa.
  2. Tengeneza mpango mpya wa kuongeza kipato k.m kuongeza muda wa kufanya kazi, kuongeza biashara.
  3. Weka kipaumbele cha kulipa madeni. Mpangilio wa kipato unachokitaka ili kulipa madeni. Njia kwa mfano, snowball, deni lenye riba ndogo zaidi. Avalanche unaanza na madeni lenye riba kubwa.
  4. Kuepuka madeni mabaya. Epuka kukopa ili kulipa madeni.
  5. Kupunguza matumizi yasiyo ya lazima. Epuka mihemko ya harambee.
  6. Tafuta njia mbadala ya kuongeza kipato chako.

Chukua hatua; kulipa deni ni tabia, tunapaswa kujifunza kuwa na tabia ya kuepuka kuingia kwenye madeni au kama tayari tupo kwenye madeni tujaribu kulipa na kutafuta njia za kuongeza kipato.

Rafiki y’all,

Maureen Kemei.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *