Misingi 10 Ya Kuwa Na Maisha Ya Furaha.

Maisha ya furaha maana yake nini? na misingi gani unaitumia ili kuishi maisha ya furaha?

Maisha ya furaha ni kuwa na amani na utulivu.

Misingi 10 ya kuwa na maisha ya furaha ni kama yafuatayo;

  1. Tegemea kukutana na watu wabaya.
  2. Ipime siku yako kabla ya kulala. Fanya tahajudi kabla ya kulala kwa kufikiria siku yako. Je, vitu gani umefanya kwa ubaya au kwa namna isiyo sahihi. Vitu gani umefanya vizuri au vitu gani utavifanya kwa utofauti siku inayofuata. Usikubali usingizi ufumbe macho yako kabla hujahesabu kila tendo ambalo umefanya. Jifokee kwa kila tendo baya na jipongeze kwa kila tendo jema.
  3. Fanya kilicho sahihi lakini usitegemee chochote. Mtu mwenye hekima hafanyi chochote kitakachomuumiza.
  4. Jijengee tabia njema. Tabia njema ndiyo zao la furaha.

Kwenye USTOA tuna tabia njema 4
A. Hekima
B. Haki
C. Ujasiri
D. Kiasi

  1. Mahusiano Bora. Ukitafuta ubaya kwa mtu tegemea kuupata lakini tusiangalie ubaya wa mtu bali tuangalie mazuri. Tuangalie namna nzuri ya kushirikiana na siyo kupingana kila wakati.
  1. Dhibiti hisia zako ili kuishi maisha ya furaha
  2. Kuwa mstahimilivu. Kushindwa na kukata tamaa visipatikane kwako.
  1. Ishi kulingana na asili. Jua unachopaswa kukifanya na ufanye hakuna chochote kilicho kibaya au kizuri. Jua unachopaswa kukifanya na ukifanye.
  1. Jua yaliyo ndani ya uwezo wako na yaliyo nje ya uwezo wako.
  2. Una muda wa kutosha kufanya chochote unachokitaka. Maisha yako ni marefu kama utafanya yaliyo mazuri

Chukua hatua; rafiki kuishi maisha ya furaha na utulivu unategemea na sisi wenyewe, hamna yeyote anayeweza kukuletea furaha ila wewe mwenyewe ujitafutie furaha na utulivu kwenye maisha yako.

Rafiki yako,

Maureen Kemei.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *