Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini kumekuwa na uhaba wa watu kufanya mambo mazuri kwa sababu wanaona hakuna anayejali.
Lakini huo siyo ukweli, mambo mazuri unayofanya, hata kama ni madogo kiasi gani, huwa yanagusa maisha ya wengine na huwa hawasahau.
Robin anatushirikisha hadithi mbili kwenye hili.
Moja ni utaratibu ambao mama yake alikuwa nao wa kumletea chakula shuleni alipokuwa mtoto. Ndani ya chakula aliweka ujumbe wa jinsi alivyokuwa anampenda. Mpaka sasa Robina anakumbuka ujumbe huo.
Mbili ni mchezaji maarufu aliyekuwa anaambatana naye ambaye alikuwa tayari kusimama pale watu walipomwomba wapige naye picha.
Alipomwuliza kwa nini ana utayari wa aina hiyo alimjibu unahitaji kufanya vitu vidogo vidogo kuwafurahisha wengine.
Na hapo ndipo Robin alijifunza umuhimu wa vitu vidogo vidogo vizuri kwa wengine, kwako inaweza kuwa kawaida, lakini kwa wengine ikawa ni kitu kikubwa ambacho hawatakisahau maisha yao yote.
Chukua hatua; hatupaswi kuchoka kwenye kutenda mema kwa wengine kwani huwa inawagusa sana na huwa wanaikumbuka kwenye maisha yao yote. Tunafaa kuendelea kutenda mema hata kama hamna anayetambua.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.