2/100 Nimejifunza LEO MAMBO MUHIMU YA KUMUOMBA MUNGU KABLA NA WAKATI AMENIINUA JUU.

  1. Anipee moyo wa Shukrani muda wote. Moyo wa Shukrani ni muhimu sana kwa sababu kushukuru ni ibada kama ni ibada basi nikikosa nitakuwa namnyima Mungu haki yake. Lakini, pia kuna vitu nitavikosa wakati bado napambana nishukuru Mungu. Siku nitaakapopandishwa juu nishukuru pia.
  2. Anipe moyo wa hekima. Hekima ya Mungu ni kitu cha msingi sana kwa hivyo niombe Mungu anizidishie hekima yake ata sasa. Hata siku nitakapo Pata hitaji langu niendelee kuomba hekima ya Mungu ili iniongoze vyema na ili isifanyike kuwa kwazo kwa watu.
  3. Anipe moyo wa unyenyekevu. Mfalme Nebukadreza Mungu alipomuinua alikuja kusahau kama ni Mungu aliye mpa cheo na umaarufu. Hadi ikafikia hatua alitumia vyombo vya madhabahuni. Hata Mwanawe Belshaza naye alishindwa kuwa mnyenyekevu pale Mungu alipo mpa nafasi ya kuwa Mfalme juu ya wakaldayo. Mwisho alikufa pasina kufaidi ikulu. Basi ili niepukane na anguko ya kuinuliwa natakiwa kunyenyekea. Hata sasa kama bado niko chini napaswa kunyenyekea zaidi ndipo Mungu atanipeleka kule kuliko na hadhina zake.
  4. Anizidishie roho ya upendo. Upendo ni muhimu sana, napaswa kuomba Mungu anipe roho ya kupenda watu nikiwa chini, nipende watu nikiwa juu. Kuwapenda watu ni ibada na amri pia, Nmejifunza kwamba kumbe nisipopenda watu nakwenda kinyume na amri ya Mungu.
  5. Anizidishie nguvu ya kushinda majaribu. Majaribu hayawezi kukoma, nikiwa chini yatakuwepo nikiwa juu yatakuwepo pia. Ombi langu moja tu Mungu anijalie nguvu za kushinda kila jaribu lijalo juu langu.
  6. Aniweke mbali na kiburi. Mfalme Nebukadreza aliangamia kwa kiburi chake baada ya kupata mamlaka kutoka kwa Mungu. Alijawa na kiburi baada kuona watu wanamtii, ana mamlaka makuu. Akasahau kuwa Mungu ndiye aliyempa mamlaka yale. Mwisho akala majani kama ngombe hivyo, niombe Mungu aniweke mbali na kiburi maana ni kubaya sana.
  7. Anizidishie roho ya huruma. Natakiwa kuwa na Roho ya huruma nikiwa chini na siku nitakapopandishwa niwe na iyo roho pia na rehema.

Rafiki yako.

Maureen Kemei

KEMEIMAUREEN7@GMAIL.COM

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *