3/100. Mbinu za kuweza kutumia akili vizuri, nilichojifunza kutoka kitabu kanuni ya siku ya mafanikio.

Kitabu hiki kimeandikwa na daktari wa binadamu, kocha wa wanamafanikio, mwandishi, mjasiriamali Makirita Amani.

Nimejifunza mengi sana kutoka kitabu hiki yakiwemo,Asubuhi ya Miujiza, nisikubali Kuendelea kupoteza maisha, mambo sapa ya kufanya kila asubuhi ili niwe na siku ya ushindi, hatua za kuondoka kwenye umaskini na mengine mengi. Lakini leo nmeamua kukushirikisha Machache miongoni mwa mengi mazuri ya kujifunza na kuweka kwenye matendo.

Njia ya Kwanza kabisa kati ya tabia ya kutumia akili vizuri ni.

  1. Kuitenga muda ambao hauruhusu usumbufu wa aina yoyote ile, na kuweka mkazo kwenye kazi yako pekee, hakuna kingine kinachoruhusiwa hapo, akili inafanya kazi kwa uwezo mkubwa kunapokuwa na utulivu.
  2. Dakika 90 za kwanza kwenye kazi kitumie kufanya kitu kimoja ndiyo muhimu kuliko vingine vyote,kitu kimoja ambacho ukikamilisha basi utafanikiwa sana. Fanya hivi siku 90 na utaona mabadiliko makubwa sana kwenye maisha yako, muhimu zaidi ni kuanzia vipaumbele sahihi.
  3. Baada ya dakika 90 za kwanza, muda unaopakia fanya kazi kwa dakika 60 na pumzika kwa dakika 10. Dakika 60 unazofanya kazi unafanya kazi kweli hakuna usumbufu wala kupeleka mawazo yako pengine, zikiisha unajipa dakika kumi za mapumziko. Linajenga umakini na ustahimilivu mkubwa kazini.
  4. Kuwa na vitu vitano vidogo vidogo ambavyo unapanga kukamilisha kila siku. Orodhesha vitu hivyo unapoianza siku yako na hakikisha unavifanyia kazi kwenye siku yako. Kukamilisha vitu vitano kila siku ni ushindi mkubwa sana kwako.
  5. Tenga nafasi ya pili ya kufanya mazoezi, kwa kuwa mazoezi Yana faida kubwa Sana kwenye mwili wako. Yanaweza kuwa matembezi tu lakini yakanufaisha sana pia yanaweza kupa utulivu na kuwa mbali na teknolojia. Mazoezi ya mwili ni sehemu ya mwili kujichaji mwenyewe. Unapofanya mazoezi mwili unazalisha nguvu zaidi ambayo unaweza kutumia kufanya makubwa.
  6. Tenga muda wa kuchua mwili wako, zipo faida nyingi za kuuchua mwili wako, Kuondoa uchovu na kuimarisha afya. Angalau mara mbili kwa wiki tenga muda wa kuchua mwili wako. Kazi unazofanya zinaweka mwili kwenye msongo ambao ukikaa Kwa muda mrefu unatengeneza magonjwa mbalimbali. Kuuchua mwili unaondoa msongo huo, hivyo hakikisha unaupa mwili huduma huo.
  7. Chuo kikuu cha barabarani. Kama unatumia zaidi ya nusu saa kwenda na kurudi kwenye kazi zako kila siku. Basi unapaswa kutumia muda huo kujifunza, kwa kusikiliza vitabu inavyosomwa au kusoma wewe mwenyewe. Usikubali kupoteza muda huo kwa kusikiliza habari au kuperuzi mtandaoni.
  8. Tengeneza timu bora, usikazane kufanya kila kitu mwenyewe, tengeneza timu bora ya kukusaidia na yale majukumu ambayo wengine wanaweza wakafanya, wape wafanye. Wewe baki na yale muhimu pekee, ambayo wewe tu ndiye unayeweza kuyafanya.
  9. Ipangilie wiki yako kabla hujaianza na kila unapolimaliza ipitie na kutafakari.Hakikisha unatumia wiki iyo vizuri na kuitathmini wiki pale unapolimaliza na kuiangalia jinsi ilivyokwenda ili uweze kuboresha zaidi wiki inayofuata.
  10. Tenga dakika 60 za kijifunza kila siku, achana na ule mda wa kujifunza asubuhi, achana na ule mda wa kujifunza ukiwa njiani.kwenye siku yako Tenga dakika 60 za kujifunza kitu kwa kina. Unajifunza kitu kitakachokuwezesha kupika hutua zaidi kwenye maisha, kazi ata biashara yako. Litakusaidia sana kuwa wa tofauti ili kupiga hatua kubwa za mafanikio.
  11. Nikimalizia kocha anasisitiza kwamba akili tayari tunazo na Mbinu za kutumia vizuri ni hizi hapa, kilichobaki ni mimi na wewe kuzifanyia kazi hili ziweze kuwa na tija katika safari ya mafanikio.Nikushukuru sana wewe ambaye umetumia muda wako kusoma maandishi haya naamini zitabadilisha mtazamo wako.Tukutane kesho katika changamoto ya siku Mia. Zimeandikwa na mimi mwelekea mafanikio, mwanafunzi na mpishi, Maureen Kemei.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *