Karibu, naendelea kukushirikisha yale ninayojifunza kutoka kitabu cha 21 lessons for the 21st century kimeandikwa na Mwana historia Yuval Noah Harari.
Kitabu hiki kimeezea kwa kina sana changamoto tunazopitia kwenye karne hii na hatua tunazopaswa kuchukua ili kuzivuka.
Mbili;changamoto ya kisiasa.
Tuliangalia Jana changamoto ya kwanza ambayo ni changamoto ya kiteknolojia. Leo tuko kwenye changamoto ya pili ambayo ni ya kisiasa.
Muungano wa teknolojia ya kibaolojia na na ya habari unaleta mtikisiko kwenye uhuru na usawa. Kwa wale ambao wana umiliki kubwa wa taarifa za wengine wanaweza kuzitumia vibaya kwa manufaa yao binafsi. Wanaomiliki taarifa Wanakuwa tabaka la juu huku wasio na taarifa wakiwa tabaka la chini.
Suluhisho lolote la changamoto za kiteknolojia lazima lihusishe ushirikiano wa kimataifa, kwa sababu kampuni ya kiteknolojia inaweza kuwa kwenye nchi moja,lakini ikakusanya taarifa za wananchi wa nchi tofauti. Mfano Facebook ipo Marekani lakini ina watumiaji dunia nzima.
Kikwazo kikubwa kwenye utatuzi wa changamoto za kiteknolojia ni mkwamo wa kisiasa na jamii. Nchi nyingi kwa Sasa zinarudi kwenye utaifa baada ya kujenga ushirikiano wa kimataifa. Mwaka 2016 ulikuwa mwaka ambao dunia iliona mambo yasiyotegemewa kutokea.
Kitendo cha Uingereza kupiga kura ya kujitoa kwenye umoja wa ulaya na Donald Trump kushinda urais wa marekani iliashiria namna ambayo watu wanafikiria utaifa zaidi kuliko ushirikiano wa kimataifa.
Sera kuu ya Trump imekuwa kuifanya Amerika kuwa bora kwa kujali mambo ya America na siyo nchi nyingine. Ushirikiano bora wa kisiasa unahitajika ili kuweza kuzitatua changamoto hizi kubwa za kiteknolojia.
Tukutane kesho rafiki tutaona changamoto nyingine inayotukumba karne hii ya 21, nikutakie siku ya mafanikio makubwa.
Makala hii imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio, ushauri nasaha na uandishi.
Maureen Kemei
Blog ;kufikirichanya.wordpress.com