Karibu, katika uendelezo wa kujifunza kutoka kitabu cha 21 lessons for the 21st century kimeandikwa na Mwana historia Yuval Noah Harari.
Yale nimejifunza kutoka kitabu hiki ni kama yafuatayo.
Kwamba kutokana na changamoto kuwa nyingi na kutokutabirika;
Watu wengi wanaishia kukata tamaa na kuona hawana cha kufanya bali kupokea hali kama ilivyo. Lakini tunapaswa kujua kwamba uwezo wetu kama binadamu ni mkubwa na tunaweza kusimama na kuzishinda changamoto zote tunazopitia.
Ili kuweza kusimama na kuzishinda changamoto hizi, lazima kwanza tuweze kudhibiti hofu zetu, tuwe na matumaini na kuwa wanyenyekevu kwa yale tunayofanya na hata kufikiri.
Moja ya vitu vinavyotupa hofu kubwa ni ugaidi na hata uwezekano wa kuwepo kwa vita ya tatu ya dunia. Lakini kwa kuangalia kwa uhalisia inagunduka ni hofu zaidi ya uhalisia.
Mwandishi anasema kwenye kitabu kuwa, ugaidi unauwa wachache Sana kwa mwaka ukilinganisha na ajali au ugonjwa sugu. Lakini magaidi wanajua hofu zetu ziko wapi na kuzitumia vizuri.
Mwandishi anatupa mfano wa jinsi magaidi wanavyokamilisha malengo yao kwa kutumia nguvu nyingine. Anatoa mfano kama Kuna mgahawa unataka kuuvuruga lakini huna nguvu, unaweza kukamilisha hilo kwa kuweka mdudu ndani ya sikio la ngombe kisha kumweka kwenye mgahawa huo. Wakati anahangaika kumtoa mdudu kwenye sikio lake, atavunja vunja kila kitu.
Hivi ndivyo ugaidi unavyoharibu taifa, kwa kuchokoza taifa kubwa na taifa hilo kuharibu taifa jingine. Mfano Marekani na Iraq.
Katika kuchagua mfumo bora wa kuendesha nchi ata jamii, mfumo wa kidunia secularism unaonekana kuwa bora kuliko mfumo wa kidini religion. Mfumo wa kidunia unaendeshwa kwa misingi mikuu sita.
Misingi ya kwanza ni ukweli
Mfumo wa kidunia unaongozwa na ukweli, na ukweli ni ule unaoweza kudhibitishwa na siyo tu kupokelewa na kuaminiwa kama ulivyo. Ukweli ni zao la ushahidi na utafiti na siyo imani.
Misingi ya pili ni kuwa na huruma.
Mfumo wa kidunia unasisitiza kuwa na huruma kwa wengine, kutambua mateso ambayo wengine wanapitia na kujali zaidi. Kwa mfumo wa kidunia huibi au kuua siyo kwa sababu dini imekataza, bali kwa kuwa unajua kwa kufanya hivyo unawaumiza wengine.
Misingi wa tatu ni usawa
Mfumo wa kidunia unasisitiza kwenye usawa baina ya watu na makundi mbalimbali. Kwa mfumo huu unajua wewe siyo bora kuliko wengine, bali kila mtu ana upekee wae unaomfanya awe bora.
Misingi ya nne ni uhuru
Mfumo wa kidunia unampa kila mtu uhuru wa kufikiri, kuchunguza na kujaribu vitu mbalimbali. Mfumo huu unaamini kwenye haki ya mtu kuwa na uhuru wa kuwa na wasiwasi, kuuliza zaidi, kupata maoni ya upande mwingine na hata kujaribu njia mbadala.
Misingi ya tano ni ujasiri wa kupambana na mfumo kandamizi na yenye upendeleo.
Mfumo huu unasisitiza kuwa na ujasiri wa kukubali kwamba hujui au umekosea. Mfumo huu unatufundisha tusiwe waoga na kupokea kitu kama kilivyo hata kama siyo sahihi, badala yake tukipinge.
Misingi wa sita ni majukumu
Mfumo wa kidunia unampa kila mtu majukumu ya kuifanya dunia kuwa sehemu bora wa kila mtu kuishi. Hawakutoa jukumu hilo na kukabidhi viongozi au mtu yeyote anageonekana ndiyo wajibu wake, bali wanajua jukumu la kuifanya dunia kuwa bora ni la kila mtu.
Tumefahamu misingi haya sita, tuyatumie katika maisha yetu binafsi na yatakuwa bora zaidi.
Mara zote kuwa tafuta ukweli, kuwa wa huruma kwa wengine, pigania usawa kwa wote, tumia vizuri uhuru wako na kuwa jasiri kusimamia kilicho sahihi na usisahau kubeba majukumu yako ya kuifanya dunia kuwa sehemu bora ya kuishi.
Imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio, ushauri nasaha na uandishi.
Maureen Kemei
Blog ;kufikirichanya.wordpress.com
Asanteh kwa misingi hii sita muhimu