Karibu, katika uendelezo wetu wa kujifunza kutoka kitabu cha 21 lessons for the 21st century kimeandikwa na Mwana historia Yuval Noah Harari.
Nikafahamu kwamba:
Kama naona kuwa navurugwa na kuzidiwa na mambo yanavyokwenda kasi duniani, basi nijue nipo mahali sahihi na angalau nina uelewa wa mambo yanavyokwenda.
Mfumo wa kidunia imekuwa migumu sana kwa mtu mmoja kuweza kuelewa namna mambo yanavyokwenda. Kuujua ukweli imekuwa ni changamoto kubwa kwa sababu propaganda zimekuwa nyingi mno zama hizi.
Katika zama zilizopita propaganda zilisambazwa kwa vyombo vya habari kama redio, magazeti, TV na hata vitabu. Hivyo watu wote walipata ujumbe mmoja.
Lakini zama hizi propaganda zinasambazwa kwa mitandao ya kijamii, hivyo kila mtu anaweza kupata propaganda inayoendana na yeye tu. Hii ni hatari sana kwa sababu watu wanazidi kugawanywa kwenye matabaka mbalimbali.
Katika matumizi yako ya mtandao ya kijamii, mfumo wa kompyuta ya mitandaoni hiyo inajua kabisa wewe unapendelea nini, uko upande upi kwa yale unayofuatilia au kushiriki. Hivyo mtu anayechagua kusambaza propaganda, anaweza kuchagua propaganda zake ziwafikie watu wa aina gani.
Ni vigumu sana kuujua ukweli katika zama hizi, hasa kama unafikiri ndani ya kundi. Huwezi kuujua ukweli ukiwa ndani ya kundi. Utaujua ukweli kwa kufikiri nje ya kundi, kwa kuufatuta ukweli kwa juhudi zako.
Hivyo kitu kikubwa tunalotoka nalo leo ni kutafuta ukweli kwa juhudi zetu wenyewe kwa kufikiri nje ya kundi.
Tukutane kesho ili tuendelee kujifunza zaidi katika kuyaelewa changamoto za zama hizi na namna tunavyoweza kutatua katika safari ya mafanikio.
Imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio, ushauri nasaha na uandishi.
Maureen Kemei
Blog :kufikirichanya.wordpress.com