34/100.ujasiri

Karibu tunaendelea kujifunza kutoka kitabu cha 21 lessons for the 21st century kimeandikwa na Mwana historia Yuval Noah Harari.

Yale nimejifunza ni kwamba:

Binadamu tumezoea kuishi kwa hadithi, kila zama zimekuwa na hadithi zake, zama za kifashisti hadithi ilikuwa nchi yangu ni bora kuliko nyingine.

Zama za kikomunisti nchi yangu inanijali na kunipatia kila ninachotaka. Zama za huria hadithi imekuwa nchi yangu inanipa uhuru wa kuishi nitakavyo.

Sasa hadithi ya huria inapotea na hakuna hadithi mpya ambayo imeshatengenezwa. Mwandishi anatuuliza kwamba, je tunawezaje kuendesha maisha kwa ubora bila ya hadithi ya nje?

Zipo njia tatu ambazo mwandishi ametushirikisha.

Njia ya kwanza ni kuwa tayari kubadilika, kuchukulia maisha kama mabadiliko na kila siku piga hatua kuwa bora zaidi. Usikubali leo iishe ukiwa kama Jana.kumbuka dunia inabadilika kila siku, ili maisha yawe bora lazima na wewe ubadilike kila siku.

Njia ya pili ni kutengeneza maisha yasiyo na hadithi, Mwandishi anasema maisha siyo hadithi, hivyo tuaje kutafuta hadithi ya kuendesha maisha yetu na badala yake tuishi maisha kwa kuyaelewa mateso. Mateso ndiyo kitu kikuu tunakutana nacho kwenye maisha, tukiyaelewa tutakuwa tumeelewa maana ya maisha yetu.

Njia ya tatu ni kufanya tahajudi. Njia pekee ya kuyaelewa mateso na kujielewa sisi wenyewe siyo kwa kufuatilia maisha ya wengine, kufuatilia habari, kuzurura kwenye mitandao ya kijamii wala kujipa kila aina ya starehe tunayotaka.

Njia pekee ni kujipa muda wa kuangalia namna akili na mawazo yetu yanavyokwenda. Kwa kuangalia na siyo kujaribu kudhibiti. Njia pekee ya kufanya hili ni kwa kutahajudi ili kuweza kuangalia akili inavyokwenda, kuyaelewa mateso na kujielewa wenyewe.

Mpendwa, tunapitia katika kipindi cha mapinduzi makubwa na maisha mapya yanakuja,ambayo yatatikisa kabisa imani yetu na hata msimamo.

Tunapaswa kuwa imara ili tuweze kustawi katika nyakati hizi za mapinduzi. Tufanyie kazi haya tunayojifunza ili mabadiliko yanayotokea yasituache nyuma.

Imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio, ushauri nasaha na uandishi.

Akupendaye ;

Maureen Kemei.

Blog kufikirichanya.wordpress.com

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

1 comment

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *