Dr ama kocha ameshirikisha njia Mingi ya kupata utulivu wakati wa changamoto fulani. Katika ulimwengu unaozidi kelele kutoka pande zote ni vizuri sana kujitafutia utulivu wa akili, Roho na mwili.
Unapopatwa na tatizo huwezi kukimbia hilo tatizo, hadi usuluhishe. Kama vile tunavyofanya wakati tunapatwa na tatizo tunajaribu kuondokana nazo kwa kutumia vilevi, ugomvi, mabishano au safari ili tu kuondoka kwenye tukio. Lakushangaza kwamba baada ya hayo yote tatizo hilo bado zinatufuata tu.
Kocha anasema utulivu ni ufunguo wa maisha.Anatushirikisha Njia za kupata utulivu katika maisha.
Utatu wa maisha ya binadamu zinazoshirikiana, akili lazima utulie ili ufikiri kwa usahihi, Roho inabeba hisia na imani, mwili unachukua hatua kwenye kile unachoamua na unachoamini.
AKILI
Ni injini ya maisha. Hili kuweza kupata utulivu wa akili lazima kuchukua hatua zifuatazo.
Kuwa kwenye wakati uliopo, kuweka wawazo kwenye kile unachokifanya na utaona mengi mazuri.
Dhibiti kinachoingia kwenye akili yako. Dr anashirikisha kwamba ni bora kukaa mbali na simu wakati mwingine na watu wasumbufu.
Safisha akili yako.kutenga muda wa kutafakari kila fikra iliyopo kwenye akili yako, na ujiulize je inamanufaa gani? Kama halina manufaa liondoe.
Tulia na fikiri kwa kina. Kocha anatushirikisha kwamba dunia ni Sawa na maji kwenye matope yaliyokorogeka, kama tunataka kuyaona vizuri, lazima tuyaache yatulie. Matatizo mengi tunayokutana nayo kwenye maisha ni kutokana na kuchukua hatua bila ya kufikiri kwa kina, kuona kitu kwa nje na kukimbilia kuchukua hatua. Tunapaswa kutulia na kufikiri kwa kina kabla ya kufikia maamuzi. Tuaje maji yatulie ili tuone kwa usahihi.
Andika. Dr anatuhimiza tutenge muda wa kuandika mawazo yetu, tunapoandika mawazo hayo tunafikiri vizuri na kuyaelewa vizuri.
Tengeneza ukimya. Kwenye ukimya ndipo tunasikia dunia inatuambia nini.
Tafuta hekima. Dr anatushirikisha kwamba chakula cha akili ni hekima, kama tunavyolisha mwili ndivyo tunavyopaswa kulisha akili.Tunaweza lisha akili kwa kusoma vitabu, kupitia watu waliofanikiwa, kujiuliza maswali magumu ili tutafute majibu. Anahimiza kwamba kadiri unavyojifunza ndivyo unagundua kwamba hujui. Muhimu zaidi anasisitiza kwamba siku utakapojiona unajua kila kitu ndipo unaanza kuanguka.
Jiamini, usiwe na majigambo. Kujiamini ni pale unapojua ndani Yako mna uwezo na kutumia. Kujigamba ni pale unapojisifia mbele ya wengine kwamba unaweza zaidi na wakati mwingine unadanganya katika kufanya hilo.
ROHO.
Zinabeba eneo kubwa za maisha yetu, tunakuwa na furaha au kutokuwa, tunakuwa na kiasi au kupitiliza, tunakuwa na kuridhika au tamaa, tunakuwa na utulivu au kukosa.
Kutengeneza utulivu kwenye roho zetu tunapswa kuchukua hatua zifuatazo.
Chagua mema. Kufanya kilicho sahihi mara zote. Kujijengea msingi wa maadili za kufuata na kujipima nayo.
Mtibu mtoto aliye ndani Yako. Dr anashirikisha kuitafakari maisha na kukabiliana na chochote tulichopitia huko nyuma. Kukabiliana na yaliyopita na tusiruhusu yaendelee kuwa kikwazo. Utulivu wa roho unakuja pale hatuna vinyongo vyovyote vile.
Jihathari na tamaa. Dr anashirikisha kwamba tamaa ni kitu mbaya, sababu haina mwisho. Kwenye kila tamaa inayoingia, anasema ni bora kukaa nayo kwa muda bila kuchukua hatua yoyote na utashangaa jinsi tamaa hiyo itakavyopita kama harufu mbaya.
Hivyo ndivyo tunaweza imarika kiroho kuweza kuyashinda majaribu tunayopitia kwa kuwa na subira na kutofanya chochote.
Tosheka. Dr anatuhimiza tutosheke na kile tunacho na tuyatumie kuyakamilisha maisha yetu. Tunahitaji kupika hatua zaidi kwa sababu tunaweza siyo kwa sababu Kuna kitu tumekosa.
Oga kwenye uzuri wa dunia. Dr anatushirikisha kutembea msituni kuona vyumbe vya Mungu vinavyoendelea na maisha bila wasiwasi. Kwa kufanya hivyo Tunapata utulivu wa kiroho na kupata msukumo wa kutekeleza majukumu.
Kubali nguvu iliyo kuu. Kuna nguvu kubwa inayoifanya dunia iende, lazima tuikubali.
Tengeneza mahusiano mazuri yanayohitaji muda, kazi na uvumilivu. Dr anasema mahusiano mazuri yanatutaka tuwe wema, waaminifu wenye kujali, kujitoa na kuwaamini wengine.
Ishinde hasira. Dr anatuhimiza tubadili hasira na chuki ziwe upendo na shukrani. Tusukumwe na upendo kwenye chochote tunachofanya maana upendo una nguvu kubwa.
Yote ni moja. Dr anashirikisha kwamba sisi binadamu wote ni kitu kimoja. Hatufai kuruhusu chochote kitutenganishe.
MWILI.
Dr anashirikisha kwamba kila tunachoweka kwenye miili yetu na jinsi tunavyotumia na kuhifadhi miili yetu, kunachangia sana kuwa na utulivu au kukosa.
Hatua za kuchukua ili kuwa na utulivu wa mwili.
Sema hapana.Dr anatushirikisha kwamba tunaposema ndiyo kwenye vitu visivyo muhimu, tunasema hapana kwenye muhimu.
Fanya matembezi. Dr anatuhimiza ni vizuri kufanya matembezi ili kuondokana n makwamo.
Tafuta upweke kujitenga kukaa peke yako kwa muda itakupa nafasi ya kufikiri vizuri,kusali na kutahajudi.
Kuwa mtu. Dr anasema unapaswa kuwa mtu saa zote, kwa kupata muda wa kupumzika, wa kutafakari, kujua ukomo wa uwezo na kuishi ndani ya ukomo huo.
Lala. Dr anasema usingisi ni riba, tunalipwa kwa kuwa na maisha.
Kuwa shujaa, Dr anatushirikisha hapa kwamba lengo la falsafa ni kujifunza jinsi ya kufa. Njia pekee ya kujifunza kufa ni kujifunza kuishi vizuri kila siku ya maisha yetu . Kuishi kila siku kama vile ndiyo siku ya mwisho wa uhai wetu.
Nakushukuru sana mwanamafanikio kwa kusoma makala haya, imeandikwa na Maureen Kemei mwanafunzi wa safari ya mafanikio na maisha na pia mpishi wa chakula kitamu.
Nikutakie siku njema tukutane kesho.