Karibu, katika kujifunza kuhusu mbinu bora za mafanikio kwenye unenaji kutoka kitabu cha ; the art of public speaking kilichoandikwa na waandishi Dale Carnegie na J. Berg Esenwein.
Tulijifunza katika somo la kwanza la kitabu hiki kuwa, njia ya kushinda hofu ni kufanya. Ya pili sasa ni kuzama kwenye somo lako.
Kitu kikubwa kinachofanya watu kupata hofu wakati wanaongea mbele ya wengine ni kuruhusu mawazo yao kuzurura kwenye mambo yasiyohusiana na kile wanachozungumzia.
Mtu anakuwa anazungumza, lakini mawazo yake yapo kwenye vitu kama watu wanamchukuliaje, je nguo alizovaa zinaonekanaje kwa watu, au akitoka hapo anakwenda kufanya nini.
Kuruhusu mawazo kuzurura ndiyo imekuwa inachochea sana hofu ya kuongea mbele ya wengine na hata kukaribisha makosa mbalimbali katika uongeaji.
Kuondokana na hali hiyo, zama kwenye somo lako, mawazo yako yanapswa kufikiria kile ambacho unzungumzia pekee. Achana na vitu vingine vyote wakati unapokuwa unaongea na fikiria kile tu ambacho unazungumzia.
Kwa kuweka umakini wako wote kwenye kile unachozungumzia, unaifanya hadhira yako nayo ipeleke umakini wao kwenye unachozungumzia na zile hofu ndogo ndogo zinapotea zenyewe.
Kama tulivyojifunza, hofu huwa inatengenezwa kwenye fikra zetu, hivyo kama utaweka fikra zako kwenye kile unachozungumzia pekee, hutakuwa na nafasi ya hofu kwenye fikra zako.
Hatua za kuchukua.
Unapopata nafasi ya kuzungumza mbele ya wengine jali kitu kimoja tu, ukweli ambao unataka watu hao waujue, mengine yote siyo muhimu kwa wakati ambao unazungumza.
Asante kwa kusoma nakala hii imeandikwa na mwana mafanikio na mshauri wako.
Maureen Kemei
Blog :kufikirichanya.wordpress.com
Maisha yangu, uchaguzi wangu.