Karibu, katika kujifunza zaidi kuhusu mbinu bora za mafanikio kwenye unenaji, katika kitabu cha the art of public speaking kilichoandikwa na waandishi Dale Carnegie na J. Berg Esenwein.
Baada ya kuwa na maandalizi mazuri kinachofuata ni kutegemea kufanikiwa. Iko ivi rafiki, kile kinachotokea kwenye maisha yetu ni ambacho tumekuwa tunakitegemea.
Sasa inapokuja kwenye kuongea mbele ya wengine, wengi huwa wanategemea kufanya vibaya. Wanajiambia watasahu, wanajiambia watakosea na mengine mengi. Na haishangazi kwa nini wanapata matokeo hayo kwenye unenaji wao.
Ili ufanye vizuri kwenye kuongea mbele ya wengine, lazima uanze ukiwa unategemea kufanya vizuri. Jione ukiwa unaongea kwa kujiamini na kwa mafanikio makubwa mbele ya wengine. Pata picha ya watu wakiwa wanakusikiliza kwa umakini na kujifunza na kukuelewa.
Unapokwenda kuongea mbele ya wengine, hicho ndiyo kinachotokea. Tofauti na ukiwa na mategemeo ya kushindwa, kila kitu kitakupeleka kwenye kushindwa.
Tunapata funzo kuwa,
Unapata kile ambacho unategemea kupata, hivyo tegemea kilicho bora na utapata kilicho bora.
Asante kwa kuchukua hatua ya kusoma nakali hii, imeandikwa na mwandishi na pia mshauri wako.
Maureen Kemei.
Blog, kufikirichanya.wordpress.com
Maisha yangu, uchaguzi wangu.
Tunapata kile tunachotegemea kwenye akili yetu asante sana