57/100. Tawala hadhira yako.

Naamini siku yako imekuwa ya mafanikio makubwa, karibu tujifunze kuhusu somo letu la mbinu bora za mafanikio kwenye unenaji. Kutoka kitabu cha the art of public speaking kilichoandikwa na waandishi Dale Carnegie na J. Berg Esenwein.

Kuihofia hadhira hasa kwa ukubwa wake ndiyo chanzo cha watu wengi kupata hofu ya kuongea mbele ya wengine. Wengi wanapokuwa mbele ya kundi kubwa la watu huwa wanajifikiria zaidi wao wenyewe kuliko wanavyowafikiria watu hao au kile wanachokwenda kuongea.

Ili kujijengea kujiamini na kuondokana na hofu ya kuongea mbele ya wengine unapaswa kutawala hadhira yako. Wewe unapaswa kuwa ndiyo nguvu kuu ambayo hadhira inafuatilia.

Utaweza kutawala hadhira yako kwa kujiamini wewe mwenyewe na kuongea kwa mamlaka. Unapoongea kwa mamlaka hadhira inakufuata. Lakini unapoongea kwa hofu na kwa hali ya chini, hadhira inakutawala na hapo utashindwa kuongea vizuri.

Ili kutawala hadhira yako vizuri, unapokuwa mbele ya wengine kuongea, jali vitu viwili pekee, kile unachoongea na wale ambao unawaongelesha. Yaani fikra zako zote zinakua kwenye ukweli ambao unataka watu waujue na watu ambao unataka wajue ukweli. Vitu vingine vyote havina muhimu.

Iko hivi rafiki, kama upo mbele ya wengine na ukaanza kujiuliza iwapo umependeza, hadhira nayo itaanza kufikiria kwa namna hiyo. Lakini unapofikia kuhusu kile unachoongea, basi hadhira nayo inaufuata kwenye hilo.

Somo kuu

Unaposimama kuongea mbele ya wengine, simama kama kiongozi na hadhira iwe inakufuata kwa kile unachozungumzia.

Asante kwa kusoma nakala hii imeandikwa na mwandishi na mshauri wako.

Maureen Kemei

Blog, kufikirichanya.wordpress.com.

Maisha yangu, uchaguzi wangu.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

1 comment

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *