Mtazamo ulionao yana mchango kubwa Sana kwenye matokeo unayopata kwenye maisha yako. Upo hapo ulipo sasa kutokana na mtazamo ambao umejijengea siku za nyuma. Na mtazamo ulionao leo, ndio utakaokujengea kesho yako.
Watu wengi wana mtazamo hasi na ambao unawazuia kufanikiwa hata kama wamejiwekea malengo makubwa na wanajua kusudi la maisha yao. Mtazamo wa wengi unajengwa na vitu vitatu ;kujiamini, kujitathmini na kujikubali.
Kujiamini ni pale mtu anapokuwa na imani ndani yake na kuona kwamba anastahili kupata mafanikio makubwa. Kama unaona hustahili huwezi ukafanikiwa.
Kujitathmini ni pale mtu anapojua kwamba anao uwezo, ujuzi na maarifa. sahihi ya kufikia lengo alikojiwekea. Kama unajidharau wewe mwenyewe huwezi kufanikiwa.
Kujikubali ni pale mtu anapokuwa na uhakika kwamba kile anachotaka kinawezekana na kipo ndani ya uwezo wake. Ukianza kuamini haiwezekani au huwezi, huwezi fika popote.
Akujaliye sana.
Maureen Kemei.
Blog, kufikirichanya.wordpress.com.