Kwenye maisha kuna kupoteza hili kupata kitu inayoitwa trade off. Yaani hili kupata unachotaka, kuna kitu inabidi upoteze.
Na kinachowazuia watu wengi wasipate wanachotaka ni kutokuwa tayari kupoteza walichonacho au wanachokipenda.
Katika kutengeneza tabia za furaha, kuna vitu lazima uwe tayari kuvipoteza. Kwenye kitabu cha ‘habits of a happy brain,’ mwandishi amegawa makundi manne ya vitu ambavyo inabidi tupoteze ili kupata.
Kwanza:muda mfupi na muda mrefu ;ili kupata furaha ya muda mrefu, lazima uwe tayari kupoteza furaha ya muda mfupi.
Pili:vyenye uhakika na visivyo na uhakika;ili kupata ambacho huna, inabidi upoteze ambacho unacho kwa sasa. Lazima uwe tayari kufanya vitu ambavyo huna uhakika navyo na kuacha ambavyo una uhakika navyo.
Tatu : mtu binafsi na kundi ;kuwa ndani ya kundi kunaleta hali ya kujisikia vizuri na kuona upo salama pia. Lakini kuwa binafsi unaweza kufanya makubwa zaidi. Kuweza kufanya yale binafsi, lazima uwe tayari kuwa nje ya kundi ulilozoea.
Nne:maamuzi binafsi na tegemezi ;kuwa chini ya utegemezi wa wengine kunakuondolea majukumu na hata baadhi ya hatari. Lakini pia kunakufanya ukose uhuru. Lazima uwe tayari kupoteza uhakika kama unataka uhuru, au kupoteza uhuru kama unataka uhakika.
Hatua ya kuchukua ;kama ambavyo tumejifunza siku ya leo, kwamba lazima tupoteze ikiwa tunataka kupata. Na mfano mzuri ni huo wa kupata furaha kama kweli tunataka furaha ya kudumu, lazima tuwe tayari kupoteza furaha ya juu juu kama ya kuzurura mtandaoni.
Na kuamua kuzama ndani katika kuwajibika kweli kwenye kazi zetu na hapo tutakuwa tunajenga furaha ya kudumu na ya kweli.
Akujaliaye sana.
Maureen Kemei.
Blog, kufikirichanya.wordpress.com