6/100.Safari ya kupata hazina yako.

Karibu sana mwanamafanikio, leo tunaangazia kitabu cha the alchemist kilichoandikwa na mwandishi Paul Coelho.

Hadithi hii inaeleza harakati za kijana mchungaji aitwaye Santiago ambaye alikuwa anapata ndoto za kutafuta hazina yake kwenye mapiramidi ya Misri. Anakwenda kuomba ushauri kwa mtafsiri wa ndoto ambaye anamwambia aende kwenye mapiramidi hayo.

Ilikuwa ngumu sana, safari yenye kila aina ya vikwazo ambavyo aliweza kuvivuka na kufika kwenye mapiramidi. Hata hivyo anajifunza kwamba hazina aliyokuwa anaitafuta haipo kwenye mapiramidi, bali kule alikotoka.

MWANDISHI KUJIFUNZA KUTOKA KWENYE KITABU CHAKE. Paulo aliandika kitabu the alchemist mwaka 1988 kwa lugha ya kireno nchini Brazil.

Mwandishi anasema kwenye wiki ya Kwanza kitabu kutoka, ni mtu mmoja pekee aliyenunua. Ilichukua miezi mingine sita kuuza nakala nyingine moja, tena kwa yule aliyenunua nakala ya Kwanza.

Ilichukua mwaka mmoja kitabu hakikuuzwa kabisa, kitu kilichomfanya mchapaji wa kitabu kuvunja mkataba wake, na mwandishi na kukabidhi kitabu chake akiuze mwenyewe.

Kipindi hicho mwandishi alikuwa na umri wa miaka 41 na alikuwa kwenye hali ya kukata tamaa. Lakini hakupoteza matumaini, bado aliamini kitabu chake kitawasaidia wengi kujua hazina za maisha yao.

Aliamua kukiishi kitabu hicho yeye mwenyewe, kwa kuianza safari ya kufikia hazina yake,kama ilivyo hadithi ya kitabu. Alitambua hazina yake ni uandishi, hivyo alichagua kuishi hazina hiyo na kuhakikisha anashirikisha hazina hiyo kwa watu wote.

Kwenye kitabu the alchemist aliandika kwamba, pale unapokitaka kitu kweli, ulimwengu mzima unafanya kila namna kuhakikisha unakipata. Hivyo alitaka kitabu chake kiifikie dunia na hapo alianza kutafuta wachapaji na wasambazaji wengine wa kitabu hicho.

Kilichapwa na kidogo kidogo kikaanza kusambaa kwa wengi. Kilianza kupata mafanikio makubwa, kikasambaa dunia nzima na kutafsiriwa kwa zaidi ya lugha nane. Mpaka leo bado ni kitabu ambacho wengi wanapenda na kukiri kimebadili maisha yao.

Kama mwandishi angekata tamaa miaka 30 iliyopita, leo hii dunia asingepata hazina hii muhimu sana.

SOMO KUBWA LA KUJIFUNZA HAPA NI.

Haijalishi unapitia ugumu kiasi gani, usiache kuamini kwenye maono au ndoto au hazina yako.

Hiki nndicho tupaswa kukipikania na dunia ukijua kweli tukitaka, basi lazima itatumia mbinu zote kuhakikisha tumekipata.

Nikushukuru kwa muda wako wa kusoma preview haya, yameandikwa na mwanafuzi wa mafanikio wa maisha ambaye anafanya kazi ya upishi. Maureen Kemei tukutane kesho majaaliwa.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *