Njia unazoweza kutumia kujifunza kuwa na fikra wazi.

Tumia maumivu kama mwongozo wa kukusaidia kufanya tafakari na tathmini ya usahihi wa kile unachoamini au kusimamia. Pale makosa au udhaifu wako vinapoguswa, unapata maumivu, yatumie maumivu hayo kuchukua hatua sahihi.

Jijengee tabia ya kuwa na fikra wazi. Maisha unayoishi, yanayokana na tabia ambazo umejijengea. Ukijijengea tabia ya kuwa na fikra wazi, kuwa tayari kujifunza na kubadilika, hayo ndiyo aina ya maisha utakapokuwa nayo.

Jua upofu wako ulipo. Angalia makosa ambayo umekuwa unafanya kwa kujirudia, pia waulize wengine wakuoneshe madhaifu uliyonayo ili uweze kuyaona na kuchukua hatua sahihi.

Kama watu wengi wanaoaminika wanasema unakosea, halafu wewe pekee ndiye unayeamini unafanya kwa usahihi, ni wakati wa kujifikiria, kuna uwekezekano mkubwa kwamba unakosea. Chukua wao na jiulize ni wapi unaweza kuwa unakosea ili uweze kuuona ukweli.

Fanya tahajudi meditate. Tahajudi inakusaidia kutuliza fikra zao, hasa kwenye nafsi yako ya chini na kukuwezesha kuwa tulivu na kuona vitu jinsi vilivyo na siyo unavyotaka wewe viwe. Tahajudi imakuwezesha kukabiliana kwa tulivu na hali yoyote, hata kama ni ngumu na kubwa kiasi gani.

Ongozwa na u|shahidi evidence – based na wawezeshe wengine kuwa hivyo. Chochote unachoamini au kukubaliana nacho kwamba ni kweli, unapaswa kuwa na ushahidi unaopaswa kuuonesha kwamba ni kweli.

Jua ni wakati gani wa kuacha kupingana na kukubaliana kulingana na mchakato uliowekwa. Kuna wakati mabishano baina yako na mwingine hayatafikia tamati, kila mtu ataendelea kuamini kwenye upande wake. Katika hali kama hii, kuendelea ni Kupoteza muda. Badala yake unapaswa kufuata mchakato sahihi, labda ya kwenda Ngazi ya juu kwa kumhusisha mtu ambaye ni mtaalamu au mwenye uzoefu zaidi.

Hatua ya kuchukua kupitia msingi huu unapaswa kuwa tayari kukabiliana na changamoto mbalimbali ili kuweza kuujua ukweli, iwe unatoka kwako au kwa wengine.

Lakini hii haimaanishi kwamba unakubaliana na wengine kirahisi, bali unakubaliana nao wanapokuwa na ushahidi wa ukweli kuliko wewe.

Akujaliaye sana.

Mwandishi, Maureen Kemei.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *