Nakukaribisha mwanamafanikio katika Kuendeleza usomaji wetu wa kitabu cha the alchemist kilichoandikwa na Paulo Coelho.
Leo tunaona wazazi wake kijana Santiago, wakimtaka awe padri ambapo ingeleta heshima kwa familia yao. Maana walikuwa Wanaishi maisha ya chini ya ukulima, ambao kila siku kazi ilikuwa ngumu na lengo ilikuwa kupata chakula.
Santiago alipowatembelea wazaziwe, aliamua kuwaeleza kusudi la maisha yake. Kwamba hakutaka kuwa padri, bali anataka kuwa msafiri.
Babaye alimweleza kuwa wasafiri ni matajiri, kwa masikini mtu pekee wa kusafiri ni mchunga kondoo. Kwa haraka Santiago alimjibu babaye kuwa anataka kuwa mchunga kondoo. Siku iliyofuata babaye alichukua akiba aliyekuwa amemwekea kama uridhi na kumkabidhi. Akamwambia itamsaidia kununua kondoo wa kuanza naye, alimtakia kheri katika safari yake.
Somo la kujifunza kwamba ipo njia ya kuishi kusudi la maisha yetu, wengi Wamekuwa wanazika kusudi la maisha yao kwa sababu mbalimbali. Wamekuwa wanaona hawana uwezo wa kuishi kusudi hilo. Santiago hakuweza kusafiri kama tajiri, lakini aliweza kusafiri kama mchunga kondoo.
HUHITAJI VITU VINGI ILI UANZE KUISHI NDOTO ZAKO.
Santiago alinunua koti, kitabu na kundi la kondoo,alihitaji hizi hili aanze safari. Koti ilimsaidia nyakati za usiku, ambazo alilala maeneo hatari. Kitabu alikisoma mchana na usiku alikitumia kama mto wa kuweka kichwa chake. Kondoo walikuwa sababu ya safari yake. Tunajifunza kwamba hatuhitaji vitu vingi ili kuanza safari yetu.
USIISHI KAMA KONDOO .
Kwenye safari yake Santiago alijifunza kitu kimoja kuhusu kondoo. Lengo la kondoo kuu ni kupata chakula na maji, wakishapata basi wanaridhika.
Kijana aligundua kitu pekee ambacho kondoo wake walijali ni chakula na maji. Akiweza kuwapatia majani mazuri na maji, basi kondoo hao waliendelea kuwa rafiki wake.
Alitafakari maisha ya kondoo hao na kuona haikuwa na tofauti, kila siku ni kuamka, kula, kunywa na kulala. Aliona kondoo hao hawajawahi kusoma kitabu kwenye maisha yao. Na hata waliposafiri, hawakuona mazingira mapya na kuyafurahia, badala yake walifikiria chakula na maji pekee.
Wengi Wamekuwa wanaendesha maisha yao kama kondoo, kila siku wanakimbizana na kazi,kwa lengo la kupata fedha ya kuendesha maisha yao. Hawapati muda wa kuyaishi na kuyafuhia maisha yao. Hawasomi vitabu na kujifunza vitu vipya. Hawasafiri na kujifunza kwenye mazingira mapya. Kwao kila siku mpya ni kama jana kutafuta chakula na maji kama kondoo.
Jambo lakutoka nalo ni kwamba tuuishi maisha yenye maana, tujifunze na kufurahia maisha. Tutapata hayo kama tutalijua kusudi la maisha letu.
Shukran sana mwanamafanikio naamini umepata kitu katika maandishi haya. Yameandikwa na mwanafuzi wa maisha na mafanikio na anafanya kazi ya upishi. Maureen Kemei tukutane kesho majaaliwa.