Jinsi ya kujizoeza unyenyekevu kunavyokufanya uwe imara.

Mnamo mwaka wa 1940,Wilma Rudolph alizaliwa kabla hajamaliza miezi tisa ambayo mimba huwa inapaswa ikamilishe kabla ya mtoto kuzaliwa. Alikuwa na pounti nne tu,hivyo alikuwa mgonjwa tangu utotoni mwake.

Akiwa na miaka minne alipatwa na ugonjwa wa polio ambapo mguu wake wa kushoto ulikunjika kwa sababu alikuwa na shida ya leg bruce.

Kwa sababu hiyo alipaswa avae viatu vya orthopedic kwa miaka zingine miwili. Kwa usaidizi wa physical therapy , Rudolph aliweza kutembea vizuri akiwa na miaka 12 na kwa mara ya kwanza kwenye maisha yake ,akajiunga na timu ya wachezaji shuleni.

Aligundua kipaji chake cha kukimbia na upendo wake kwenye mchezo huo,alianza kufanya mazoezi. Akiwa na miaka 16,alipata nafasi kwenye uchezaji wa timu ya Olimpiki mwaka wa 1956. Akiwa mchanga kabisa kwenye timu hiyo alishinda medali kwa mbio iyo ya 4×100 relay. Baada ya hapo alirudi nyumbani na akazidi kufanya mazoezi zaidi kwa ajili ya Olimpiki ijayo.

Mwaka wa 1960 ,alijiunga na chuo kikuu cha Tennessee state ambapo aliweza kuendeleza mazoezi yake. Kwenye mwaka huo huo wakati wa mchezo wa Olimpiki, Rudolph akawa mwanamke wa kwanza nchini Marekani kushinda medali tatu ya gold kwenye Olimpiki moja. Alisifiwa sana na akawekwa kwenye historia, Rudolph alipumzika kutoka kwenye mchezo wa kukimbia akiwa na miaka 22.

Hata kama watu wengi wanalaumu shida na matatizo walizopitia wakiwa wadogo, Rudolph hakuwa hivyo. Hakupa nafasi chochote kimzuie hata ugonjwa ambao ulimsumbua tangu alipozaliwa. Hata hakulaumu uweusi wake kama mwanamke mweusi Marekani, au hakulaumu ufukara kwenye familia yake uliokuwa haujiwezi. Hata hivyo alijua kwamba dunia haiwezi ikamzuia yeye kufanya kile alichokipenda.

Rudolph alisema kuwa “haijalishi ni nini unataka kukamilisha,kikubwa ni nidhamu unayokuwa nayo. I was determined to discover what life held for me beyond the inner city-streets .” Hivyo ndivyo Rudolph alivyoenda tangu akitembea na mguu uliyowekwa pandeji hadi aliposhinda medali ya Olimpiki kwa muda wa miaka mitano tu.

Rudolph alipofariki mwaka wa 1994, legacy yake nzuri bado inaishi hadi sasa na bado inaendelea kuwapa wakimbiaji wengine tumaini waliopo na wajao.

Kuendelea kudhania kwamba umeumbwa Ili upate zaidi ya ulichonacho sasa haiwezi ikakusaidia chochote kwenye maisha yako. Unapoteza muda, uwezo wako inaweza kufanya ufe moyo mapema.

Unapochukua hatua ya kuacha kujionyesha ,na ukawa tayari kujifunza ,utakuwa tayari kujiboresha. Hivyo itakusaidia kwenye ufanisi wako kazini na kwenye maisha kwa ujumla.

Unapoacha hali ya kuona kwamba unataka zaidi na ukatosheka na kile ulichonacho, utapata mafanikio makubwa. Utaweza kusonga mbele kwa amani bila kuwa na msongo wowote. Kwa sababu utaona umetosheka lakini unatafuta mafanikio zaidi bila kuhisi uchungu wala kukata tamaa.

Mwandishi wako.

Maureen Kemei.

http://www.uamshobinafsi.com/wp-admin

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *