Jinsi ya kufanya uzoefu wa kuvumilia ukimya.

Wengi wetu tumezoea sana kusikia kelele nyingi kutoka pande zote. Hata inafika wakati mwingine watu wanatafuta njia mbalimbali za kuwafanya wasipaki peke yao wakiwa wametulia na mawazo yao.

Mtu yeyote anayelala wakati Tv ama redio inaongea , ukijaribu kuweka mawazo yako sawa , wakati unasikiliza kelele nyingi,hivyo sio afya nzuri kwako.

Kutengeneza dakika chache ya utulivu kwenye siku yako itakusaidia kwenye kuongeza nguvu zako . Chukua dakika kumi kila siku ukiwa umekaa chini huku umetulia na usijishughulishe na chochote bali unatulia huku ukifikiria.

Kama umezoea kelele na shughuli nyingi za kelele,kukaa kama umetulia kinaweza kusikuwe kuzuri sana kwako mwanzoni,lakini kwa kufanyia mazoezi kila siku kutakuwa sawa.

Unapaswa kuitumia wakati wa utulivu kufanya mambo yafuatayo:

Kwanza unapaswa upitie malengo yako. Unachukua dakika chache kila siku kufikiria kuhusu malengo yako. Fanya tathmini ya jinsi unavyoendelea na pia kutafakari namna unavyoweza kujifanyia maboresho au mabadiliko unayohitajika kufanya.

Pili zingatia hisia zako,fikiria kuhisi hisia zako na usongo wako wa mawazo. Chunguza kama ziko sawa ili uweze kutafakari njia za kuweza kujiboresha.

Tatu ni kuweka malengo yako wazi. Kamwe usiache kuota ndoto kubwa kuhusu kile unachohitaji, jinsi unavyotamani kesho yako kiwe. Njia rahisi ya kutengeneza kesho yako sasa ni kuamua aina gani ya maisha unahitaji.

Nne ni kwenye kuandika jarida lako. Uandishi wa journaling ni nzuri sana kwa sababu itakusaidia kuelewa zaidi na kujifunza kutoka kwenye hisia zako. Tafiti zinaonyesha kwamba kuandika kuhusu uzoefu wako wa kila siku na hisia zinazozunguka uzoefu wako zinakusaidia kwenye kuimarisha kinga za mwili na pia zinapungua msongo wa mawazo na pia kusaidia afya.

Tunaishi katika dunia ambayo kila siku tunaunganishwa na watu tofauti. Lakini kuunganishwa huku kitijidali inamaanisha kwamba tunapata fursa chache sana ya kukaa peke yetu na fikra zetu .

Kufikia simu yako ya mkononi na kuperuzi mtandaoni inachukua muda wako mwingi. Kuchukua muda wa mapumziko na kuacha kutumia teknolojia na kuweka muda mwingi kwenye kukaa kimya kwenye siku yako Kwa kujaribu kufanya yafuatayo;

  1. Kuzima Tv Yako kama unatumia
  2. Kuendesha gari yako bila kusikiliza redio.
  3. Kufanya matembezi bila simu yako ya mkononi.
  4. Kufunga eletroniki zote wakati mwingine na kupumzika.

Utulivu ni muhimu sana kwenye maisha yetu ya sasa ,kwa sababu utapata muda mzuri wa kutafakari maisha yako ,kuweka vizuri malengo yako na kuweza kujua dosari hivyo kujifanyia marekebisho mapema.

Mwandishi wako.

Maureen Kemei.

http://www.uamshobinafsi.com/wp-admin

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *