Jinsi ya kujichumbia wewe mwenyewe.

Kupanga tarehe yako solo.

Kifunguo pekee cha kujitengenezea muda wako mwenyewe ni kwamba,unapaswa ukafanye maamuzi hayo wewe mwenyewe,yaani yawe yanatoka ndani yako kabisa.

Wazee wengi wamezoea kuishi peke yao licha ya kwamba jamii wanawaepuka kwa mfano; wazee hao wana uwezekano mkubwa wa kukaa peke yao kwa utulivu, bali sio rahisi wafaidike zaidi na hiyo hali yao ya upweke.

Lakini kwa watu ambao wako’bize’ ambao wanahusiana na wengine kila mara,kwao kuweka muda wa kuwa peke yao inakuwa ni fursa nzuri ya mapumziko na pia ya kujifanyia maboresho.

Ikiwa jambo la kuwa peke yako haikufuraishi, unapaswa uelewa kuwa ; kuwa peke yako ni ufunguo sahihi wa kutengeneza uzoefu chanya wa upweke huo. Kwa kutumia dakika chache ya ukimya unapaswa utumie vizuri muda huo kujichumbia mwenyewe hata kama ni mara moja kwa mwezi.

Kwa kujichumbia hivyo inakukumbusha ujifanyie kitu chenye tija kwako. Sio kwa sababu unakosa watu wa kujumiana nao ,bali ni kwa manufaa yako mwenyewe.

Kuna tafiti uliofanywa mwaka wa 2011,ulidokeza kwamba ‘ An exercise to teach the psychological benefits of solitude.’ Yaani watu wanaojichumbia wenyewe wanapata utulivu na ukimya na pia wanafurahia uhuru wa kufanya kile wanachotaka bila kuruhusu usumbufu wowote ule au kutarajia mambo fulani.

Wachache ambao hawakupata fursa ya kufurahia upweke huo wa kuwa peke yao,hawakuweza kufurahia uhuru huo wa utulivu. Lakini unapoongeza muda wa utulivu kwenye siku yako utafurahia na utapanga muda wa utulivu na ukimya kila mara.

Wakati wavuvi wanapovua samaki katikati mwa bahari ,huo ni muda mzuri sana kwao wa kupata amani na pia wa kufanya upya mawazo na fikra zako . Wengi wanakataa uzoefu huo na kuona kuwa ni wa kutosha sana .

Kwa kudharau kitu hutaweza kukaa nayo kwa muda mrefu. Ni muhimu kujishughulisha na mambo yanayoleta upweke kwenye maisha ambayo utafurahia kwenye kila siku ya maisha yako.

Kama unapenda asili, unapaswa uzingatie kutumia muda mwingi kwenye kufurahia mazingira na pia kutembea kwenye mapori. Kama unapenda chakula kizuri,unaweza ukapiga au uende kwenye mkahawa unaoupenda.

Hupaswi kukaa nyumbani tu ndio ufurahie upweke,badala yake chagua kufanya kitu ambacho huwezi ukafanya ukiwa na watu. Hakikisha haupo kwenye vitabu tu au unachati na mwenzako. Pointi nzuri hapa la kujichumbia mwenyewe ni kuhakikisha unakuwa peke yako na mawazo yako.

Mwandishi wako anayekujali sana.

Maureen Kemei.

http://www.uamshobinafsi.com/wp-admin

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *