Kuzama kwenye mawazo ya zamani ni kama utambuzi,lakini mwishowe inashawishi hisia na tabia .Kwa kubadilisha namna unavyofikiri kuhusu mambo yaliyopita,inakupa fursa ya kusonga mbele zaidi.
Tengeneza muda wa kufikiri kuhusu yaliyopita,wakati mwingine akili zetu zinahitaji fursa ya kutatua mambo na wakati mwingine na kadri unavyojiambia kwamba hutaki kufikiria kuhusu mambo hayo,ndivyo yanavyokuja kila mara. Badala ya kun’gang’ana kufutilia mbali mawazo hayo unaweza ukajiambia nitafikiria kuhusu hayo baada ya dinner. Alafu ujipe dakika tano ya kufikiria kuhusu kitu hicho. Wakati wa kufikiri ukiisha endea na kingine au ujipe wazo jingine jipya la kufikiria.
Tengeneza mpango itakayokusaidia kufikiria kuhusu kitu kingine, kwa mfano amua kuwa unapofikiri kuhusu iyo jambo au kazi yako ambayo hukufanikiwa nacho,utabadilisha fokasi yako kwa kufikiri kuhusu mipango yako au likizo yako inayofuata. Hii inakusaidia kukabiliana na fikra hasi kabla hujaenda kulala.
Weka malengo yako ya mbeleni . Haiwezekani fikra zako mara zote ni za zamani kama unapanga za mbeleni,. Unapaswa uweke malengo ya muda mfupi na mrefu alafu uchukue hatua inayohitajika Ili kufikia malengo yako . Hii itakupa kitu cha kuangalia mbele hivyo kukuzuia kwenye kufikiria ya zamani.
Mawazo yetu siyo ya kweli kama vile tunavyofikiri . Mara zote tukikumbuka nyakati mbaya,tunaongezea na kufanya kuwa changa kubwa. Kama unafikiri kuhusu kitu ulichosema kwenye mkutano kisha ukajutia ,utaona kuwa watu walikuhukumu vibaya. Ukikumbuka mawazo hasi,jaribu mikakati hizi Ili kuweka mazoea yako vizuri.
Weka fokasi yako kwenye funzo unachopata. Kama umepitia nyakati ngumu inabidi uweke fokasi yako kwenye yale unayojifunza kutoka kwenye mazoea yako . Kubali kuwa ilifanyika na ufikirie kuhusu jinsi utakavyokuwa mtu wa tofauti uliyebadilika. Kwa sababu ya hayo,kumbuka kuwa siyo lazima iwe kitu kibaya . Labda ujifunze kuongea kwa sababu uliona kama watu wanakuona wewe ni wa chini ama unajifunza kuwa wa kuaminiwa ukitaka mahusiano ya dumu. Wakati mwingine tunajifunza kutokana na wakati mgumu unm
Mawazo yako yajengwe kwenye mantiki wala sio hisia. Kufikiria yaliyo hasi mara nyingi inasumbua sana kwa sababu utaweka fokasi kwenye jinsi unavyohisi wakati wa tukio fulani. Lakini ukijikimbusha tukio hilo kupitia mantiki masumbuko yote yatapungua. Badala ya kufikiria kuhusu yaliyopita ulivyohisi ulipoenda mazishi kumbuka yote kuhusu tukio hilo; pahali ulipoketi ,nini ulijifunza ,nani alikuwepo hapo . Unapofikiria kutoa hisia za mahali hapo haitakusumbua sana.
Kuwa na matazamo wa tofauti kuhusu hali. Ukiweza kutafakari yaliyopita. Chunguza njia zingine zinazofanana ,unatawala jinsi unapokumbuka habari iyo . Habari iyo inaweza ikasambazwa mara nyingi na bado ikawa kweli . Kama ulivyosasa yanastua unaweza ukajaribu njia nyingine.
Tunapaswa kuepuka kufikiria kuhusu mambo yaliyopita na mara nyingi mawazo yetu yawe kwenye wakati uliopo . Tukifanya hivyo tutaweza kupunguza magonjwa mengi yanatokana na kufikiria magumu tuliyopitia, jinsi tulivyoumizwa na mengineyo.
Mwandishi wako akupendaye sana.
Maureen Kemei.
http://www.uamshobinafsi.com/wp-admin